TANESCO kuweni wakweli kwamba umeme umepanda bei

Hizi ndio bei halisi za umeme toka mwaka 2016 hivyo tuendelee kupokea taarifa sahihi
Mtu anaweza kutolewa kutoka tarrif moja kwenda nyingine endapo atazidisha matumizi mfululizo kwa muda gani?
 
Mimi Nikiri Tanesco Kwenye Watumiaji Wa Umeme Ambao Hawazidi Unit 75
Mtu Akienda Kwenye Ofisi Zenu Za Wilaya, Mkoa, Mmekuwa Mnakataa
MMajibu Y anayotolewa Ndiyo Kama Mleta Mada Alivyosema

Utaambiwa Huduma Hiyo Haipo Hata Ukiandika Barua Hawaipokei
Sasa Unajiuliza Kwanini Mnakuwa Na Ndimi Mbili
Unachosema Jukwaani Kingine, Ukifika Kwenye Ofisi Zenu Kingine
 
Naomba tu niwe shuhuda kuwa Mimi nipo Dar na nilisota karibia miaka miwili kuomba hii huduma enzi za Chato bila Mafanikio. Ila mwaka huu mwanzoni nilienda kuomba na ndani ya wiki wakanibadilishia. Sasa hivi najiachia tu
 
Nikonekt mambo safiii, Ahsante kwa ushuhuda mzuri
 
Tafadhali onesha namba ya mita kwa maelezo sahihi
 
na hizo ndo kauli zao huku mikoani. maana mimi nina miezi mitatu. nilivyoenda kuulizia utaratibu wa kubadilishiwa nikajibiwa kwamba hiyo huduma haipo kwa mijini
 
Nipo usa river Arumeru, matumizi yangu hayajawahi kufika unit 75 tangu niwe na umeme nyumbani zaidi ya miaka 9, Mwezi uliopita yaani Juni 2021 nimebadilishiwa matumizi kuwa ya juu baada ya kupata meseji ya keychange na mabadiliko kuanzia hapo, Kwa sababu ulizotaja hapo usa river napo ni mjini?
 
Tafadhali onesha namba ya mita kwa maelezo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…