Hatimaye Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inaenda kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme unaofikishwa mgodini hapo
Kituo hicho kilichojengwa kwa gharama ya Sh60.6 bilioni kitakuwa na uwezo kupooza umeme wa msongo wa kilovoti 33 kuwa kilovolt 11 ndani ya mgodi wa GGML na kina uwezo wa megawati 40.
Kampuni nyingi za madini tangu miaka ya 2000 hutumia umeme wanaouzalisha wenyewe, sasa Serikali imekuwa na jitihada za makusudi kufungamanisha sekta ya nishati na sekta kubwa za uzalishaji kwa kuzalisha umeme unaotosheleza mahitaji ya wawekezaji wakubwa.
GGML hutumia megawati 40 ambazo huzalisha kwa mafuta ya dizeli lakini sasa kufikisha umeme wa Tanesco katika mgodi wa kampuni hiyo unaenda kupunguza gharama za uendeshaji kwa asilimia 50, ambapo wataokoa Dola za Marekani milioni 19 kila mwaka. Pia Tanzania tutapunguza hewa ya ukaa kilotons 81 kufikia 2030,"