Nilijisajili kuunganishiwa umeme ikiwa ni kuletewa nguzo 2. Nikatumiwa control number ya malipo baada ya kufanya survey kuwa nitume Tsh 697,000/=. Mpaka muda huu ujumbe ni ule wa mwanzo tu kuwa malipo yako yanashughulikiwa na utapokea ujumbe mfupi kuthibitisha malipo yako. Siku ya 2 hakuna uthibitisho wowote nimeupata, hii maana yake nini, pesa zangu zimepotea hewani? Kuna faida gani ya kutumia mfumo wa computer si bora tungeenda kulipa ofisini km mwanzo? Au watumishi wa TANESCO wanahujumu mfumo wa serikali kwa maslahi yao? Mh. Waziri labda utusaidie. Nchi hii bila viboko maofisini ni ngumu kubadilika. TANESCO naomba nijulisheni km hela yangu imepotea mnakojua nyie