TANESCO live betting

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Sisi wenye macho ya fursa tumeona ipo fursa hapa.
Imagine unaanzisha live betting ya kukatika kwa umeme.
Masharti ni mkeka unawekwa kila siku saa sita kamili usiku.

Mkeka unadumu masaa 24.

Mteja anatakiwa kubashiru mahali alipo Umeme utakatika mara ngapi kwa siku.
Kiwango cha kuweka kwenye mkeka kinaanzia tsh 500,na kuendelea

Odds ziwe kama hivi
1. Umeme utakatika mara moja =×10

2.Umeme utakatika zaidi ya mara moja lakini sio zaidi ya mara 3=×25

3.Umeme utakatika zaidi ya mara moja lakini sio zaidi ya mara 5 =× 50

4.Umeme utakatika zaidi ya mara 5 lakini sio zaidi ya mara 8=×75

5.Umeme utakatika zaidi ya mara 8=×80

6.Umeme utakatika siku nzima=× 200

Nitaweka mawakala kila wilaya kudhibiti udanganyifu.

Mfano mtu akaweka tsh elfu 10,000 akasema umeme utakatika siku nzima atajishindia tsh 10,000× 200= tsh 2,000,000/=

Mnaonaje hili wazo,je sheria inaruhusu?, Brela watakubali?

Karibuni kwa maoni na ushauri

Mwisho kabisa nimshukuru mama kuniwezesha kuandika hapa.
 
Bonge la idea 💡
 
😅😅😅🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…