Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
"....Kihansi, Hale na Bwawa la Mungu yote yamekumbwa na uhaba wa maji hali inayopelekea mchana kutozalisha umeme ili kujaza maji ili usiku uzalishaji ufanyike."
TANESCO.
=======
Mamlaka ya Hali ya Hewa hivi karibuni ilitoa taarifa juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoleta athari nyingi ikiwemo upungufu wa vipindi vya mvua unaopelekea hali ya ukame na kuongezeka kwa joto nchini. Hali ambayo imeendelea kujitokeza nchini na katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Mnamo mwaka jana tayari Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) lilishaanza mikakati ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mseto vya nishati. Mpaka sasa mradi wa kituo cha ubungo namba 3 chenye uwezo wa megawati 112 kinachozalisha umeme kwa gesi umekamilika. Mradi wa kinyerezi 1 extension ambao utaingiza jumla ya megawati 185 katika gridi ya taifa unatarajia kukamilika hivi karibuni. Mradi wa umeme unaotokana na nguvu za jua mkoani Shinyanga, Kishapu ukitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka 2023 ukiingiza megawati 50 kati ya 150.
Pamoja na hayo Shirika limeendelea na mikakati ya kuhakikisha tunaongeza vyanzo vingine vya uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo vya nishati jadidifu ambapo hivi karibuni tumeingia makubaliano na kampuni ya Masdar yenye makao yake Abudhabi Jijini Dubai. Ushirikiano huu unalenga kuwezesha miradi mbalimbali ya umeme jadidifu utakaofikia megawati 2000.
Ni dhahiri kwamba, kama mipango hii isingeanza kutekelezwa pengine hali ya kupatikana kwa umeme ingekuwa mbaya zaidi tofauti na ilivyo sasa. Hata hivyo, ni maeneo kadhaa tu katika baadhi ya mikoa ambayo yataathirika katika nyakati tofauti na tutaendelea kuwataarifu wateja wetu kadiri miradi hii itakapoanza kuingiza umeme katika gridi.
Shirika linawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu unaoweza kujitokeza na linawahakikishia kuwa litaendelea kutoa taarifa mbalimbali za hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme.