Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Wadau, salaam!
Mi nipo kanda ya ziwa. Nina kiduka, ambacho kinafanya shughuri za ki fedha, yaani, wakala wa Benki mbali mbali, na pia, makampuni ya simu. Pamoja na wateja wa kutoa na kuweka fedha, wapo wa kununua Luku, pamoja na kulipia maji.
Sasa, toka mwezi huu wa Septemba uanze, nimekuwa nikiwasikia wateja wa kununua umeme wanalalamika, kuwa hawapati umeme kwa fedha waliyokuwa wakinunulia miaka yote, yaani kwa wale waliokuwa wamepata punguzo, kwa kuelezwa kuwa serikali imewawekea ruzuku.
Mabadiliko hayo, binafsi nilikuwa sijui, jana Jumapili, ndiyo nilipata nafasi ya kukaa hapo shughurini kwangu, ndipo nilipojithibitishia kuwa, kwa sasa bei ile haipo, kwani watu wote, niliokuwa nafahamu wapo kwenye ile punguzo, kila waliponunua, hawakaupata unit walizokuwa wanapata.
Sasa Wakuu, kuna tanzazo lililotolewa na Serikali, au TANESCO kwa mabadiliko hayo? Kama lipo, naomba nami nilisome, ili nami niwawekee wateja, ili maswali kwa sisi tunaowauzia yapungue!