“Ipo siku mtanikumbuka, sio kwa mabaya yangu; bali mazuri yangu” JPM.
Inabidi upate changamoto ujue tofauti ya jambo jema na baya.
Miaka mitano ya umeme wa uhakika halafu muhusika wa usimamizi wanasiasa uchwara walikuwa wanadai anaua biashara na uchumi.
Halafu hawa wanaouwa biashara na tuzo wanapewa na mafisadi,
Nchii kufuata mkumbo wa wanasiasa kwa hoja zao za majungu utajikuta pabaya sana, wakati wanufaika ni wengine kabisa.
RIP Magufuli
Unakosea ku - generalize mambo.
Si kwamba Hayati JPM alikuwa mbaya totally. Alikuwa na uzuri wake kwa kiasi kikubwa sana. Lakini pia alikuwa na ubaya (udhaifu) wake mkubwa pia.
Mathalani, kwenye eneo hili la umeme alikuwa mzuri. Lakini huwezi kujenga uchumi wa nchi kwa kuangalia na kutilia mkazo push factor moja tu ya kiuchumi..
Lakini, ni kweli pia alikuwa anapiga vita sana watu wenye fedha (matajiri) kwa dhana kwamba ni wezi na mafisadi..
Na kwa kutumia dhana hii (ya kudhani tu), wasaidizi wake serikalini wakautumia mwanya huu kumuonea na kumnyang'anya fedha yeyote na sio kwamba ziende serikalini kama mapato bali ziliingia kwenye mifuko binafsi ya viongozi hawa.
Huu ndiyo tuliuita ujambazi au wizi wa kidola....
Liko eneo jingine ambalo Hayati Rais JPM alivurunda sana -
Eneo la ujenzi wa demokrasia huru, na ya ushindani wa haki...
Nadhani ni kwa sababu ya asili yake ya
ubinafsi mkubwa na
ulafi wa madaraka aliokuwa nao tangu akiwa mbunge kule Chato na hivyo kufanya kuwa kiongozi mwoga na asiyejiamini.. Kiongozi mwenye sifa na tabia hizi siku zote akipewa madaraka makubwa, huishia kuwa dikteta tu. Ndivyo alivyokuwa huyu ndugu yako...
Mimi binafsi, mwanzoni mwa utawala wake kati ya 2015 hadi 2017 nilikuwa nampenda sana pamoja na mapungufu yake by then....
Lakini nilikuja
kumdharau na kumuona kumbe ni kiongozi mmoja
mjinga na
mpumbavu aliyepindukia pale serikali yake ilipofanya jaribio la kumuua mwanasiasa machchari na mkosoaji mkubwa wa utawala wake pamoja chama kinachoongoza serikali hata sasa CCM ndugu
Tundu Antipasi Mughway Lissu wa CHADEMA..
Watu huuliza Kuna uthibitisho gani kuwa Rais na serikali yake walihusika?
Daima hili swali huwa linatoka kwa wajinga na wapumbavu pekee wasioweza kutumia vyema vichwa vyao vyenye akili kufikiri na kuchakata mambo...
Ushahidi kuwa Hayati Rais JPM na serikali yake wanahusika ni wao wenyewe (serikali) kwa kutumia mamlaka za uchunguzi kushindwa kujisafisha na tuhuma hizi kwa serikali kufanya uchunguzi
makini na wa
wazi kwa kila mtu wa tukio hilo baya kabisa kwa mwanasiasa na mbunge wa kaliba ya Tundu Lissu kupigwa risasi zaidi ya 35 mchana kweupe ktk maeneo ya viongozi tena akitoka kazini...
Yaani hakuna uchunguzi wowote mpaka sasa kwa visingizio lukuki visivyo na vichwa wala miguu...!!
Ktk mazingira haya, ni nani mwenye akili timamu anaweza kuwa na shaka na uhusika wa Rais na serikali yake..?
Honestly, mimi, tangu wakati huo hajawahi kuwa moyoni mwangu regardless alifanya nini..!