Tanesco msituchezee akili -- maboresho yenu ya LUKU yamekwama!

Imani na tanesco ilishakufa kitambo sana
 

nimenunua kwa wakala baada ya kuona foleni ni kubwa pale tanesco mikocheni lakini nilipoingiza kwenye luku ikakubali, nikagundua kwa wenye mita za vichochoroni a.k.a za vishoka ndio zinagoma mpaka ufike kwenye ofisi zao
 

well said!!
watanzania wengi ni tu wazembe, tunapenda kulalamika, tunapenda mteremko, maneno mengiiii.
taasisi zote zipo hivyo.wafanyakazi wengi wapo hivyo.kila mtu ajirekebishe.
 
Tumechoka walopitisha hizo dill n kutuachia uchafu wao wanakula kuku kwa mrija namaluku yao ya dezo kibao eeh mwenyezi mungu nipe nchi hii kuiongoza kwa miezi sita tu
 
Leo asubuhi nilikuwa kwenye mstari pale Ilala Petrol station kwa wakala wa LUKU nikashuhudia watu kibao wakilalamika kwamba baada ya maingizo ya zile seti mbili za namba, maingizo ya umeme hayaingii. ilipofika zamu yangu ya kununa nikaenda nyumbani, lakini baada ya kuingiza seti zile mbili zanamba, manunuzi ya umeme yaliktaa kuingia. Nikarudi kwa wakala na nikakuta watu kibao zaidi wakilalamika hivyo hivyo.

Tanesco toeni jibu kwa haraka. Au wanaringia hiyo monopoly waliyo nayo na ndiyo maana hawajali kitu?
 
Nafikiri Tanesco kuna kitu wanafuatilia kama si kuweka mfumo mpya. Tusilalamike sana, kama umenunua umeme kwa njia walizosema na ukapata tatizo lolote, wapigie simu maana number zao zipo kwa kila agent wa Tanesco.
 
Hivi tutaacha lini kulalamika? Tuwapeni muda jamani, haya mambo yatarekebishwa tu! Ila kama mita yako ni ya vishoka itakuwa imekula kwako!
 

Mimi yamenikuta hayo niliambiwa kwamba nikinunua napata karatasi 3 lakini nilipewa karatasi moja na dada muuzaji nikamuuliza mbona kuhusu karatasi 3 akaniambia usiwe na wasiwasi ukiingiza utaingia kufika home nikaambulia patupu kurudi akanipa namba nipige hiyo namba ipo bize kuanzia jana asubuhi mapka napoandika ujumbe huu. inaonekana tanesco hukurupuka kwenye kila kitu wanachotaka kufanya.
 
Mimi nilipata karatasi 3. Na 1 na 2 zilionyesha ch1 na ch2 lakini ya 3 ikawa rejected
 
heri nyie mliopata huo umeme, mie foleni iliyopo imebidi niahirishe kutumia umeme mwezi huu, hapa najaza mafuta ya taa kwenye chemli zangu maandalizi ya giza usiku
 

Mimi sikupata vikaratasi vitatu na siko matatani. LUKU ilifanya kazi vizuri tu. Nahisi kuna mita za zamani na za sasa. Za zamani ndo unapata vikaratasi vitatu na za sasa unapata kikaratasi kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…