TANESCO na Serikali walipeni watu fidia wahamishwe Rufiji. Bwawa la Umeme ni muhimu. Kila Mtanzania achangie fidia kwa kuongezewa 1000 kwenye Luku

TANESCO na Serikali walipeni watu fidia wahamishwe Rufiji. Bwawa la Umeme ni muhimu. Kila Mtanzania achangie fidia kwa kuongezewa 1000 kwenye Luku

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
1,340
Reaction score
5,588
Bwawa la umeme Rufiji ni muhimu sana kwa nchi nzima. hivyo tunapaswa wa Tanzania wote kulilinda bwawa lisibomoke kwa kuchangia pesa za fidia ya kuhamisha watu wote wa rufiji maana umeme tunautaka wote Tanzania nzima

1712766682229.png

Hali ya rufiji ni mbaya.

nawaza tu kwa nini serikali isiwahamishe wakazi wa rufiji.

Hela za kuwaamisha zichangiwe na watumiaji wa umeme wote Tanzania.

Kila kaya inayotumia umeme ichangishwe elfu moja maarufu kama buku. Hela hizo zipelekwe rufiji na kuwalipa watu fidia.
 
Vipi unaandika ukiwa hapo katikati ya hayo mafuriko? Kaa utulie ueleweke sio wanaJF wote wanaishi Rufiji

ni kweli ila Bwawa la umeme halitumiwi na wanaoishi rufiji peke yao.

mpaka wa Tanzania wa Mbeya, Mwanza, na Bukoba na wao wanafaidika na umeme wa bwawa la rufiji.

hivyo wanapaswa kuwajibika kulilinda bwawa
 
Bwawa la umeme Rufiji ni muhimu sana kwa nchi nzima. hivyo tunapaswa wa Tanzania wote kulilinda bwawa lisibomoke kwa kuchania fidia ya kuhamisha watu wa rufiji maana umeme tunautaka wote Tanzania nzima

View attachment 2959912

Hali ya rufiji ni mbaya.

nawaza tu kwa nini serikali isiwahamishe wakazi wa rufiji.

hela za kuwaamisha zichangiwe na watumiaji wa umeme wote Tanzania.

kila kaya inayotumia umeme ichangishwe elfu moja maarufu kama buku. hela hizo zipelekwe rufiji na kuwalipa watu fidia .
Sema watz tunapenda sana michango aisee.

Hebu acha hayo mawazo yako basi.
 
ni kweli ila Bwawa la umeme halitumiwi na wanaoishi rufiji peke yao.

mpaka wa Tanzania wa Mbeya, Mwanza, na Bukoba na wao wanafaidika na umeme wa bwawa la rufiji.

hivyo wanapaswa kuwajibika kulilinda bwawa
Kwani walioondolewa kupisha ujenzi wa bwawa, si walishalipwa fidia? Hawa wanatoka wapi?
 
Hivi kwanini tusianzishe kibubu cha Taifa, yakitokea majanga tunatoa kwenye kibubu
 
Kwani walioondolewa kupisha ujenzi wa bwawa, si walishalipwa fidia? Hawa wanatoka wapi?

Bwawa lilipojengwa ni sehemu ambayo haikuhamisha watu.

watu wanapatikana kwenye maeneo mbali na bwawa lilipo. ila ndio njia ya maji yanayotoka kwenye bwawa kwenda baharini
 
Naunga mkono.Ila wakihamishwa,maeneo yao mapya yapimqe ili uzaliwe mji wa kisasa.Kama serikali itashindwa kupima.Basi wawaelekekekeze wananchi wenyewe wajipimie na kujenga miji yalo kwa mpangilio
 
Bwawa lilipojengwa ni sehemu ambayo haikuhamisha watu.

watu wanapatikana kwenye maeneo mbali na bwawa lilipo. ila ndio njia ya maji yanayotoka kwenye bwawa kwenda baharini
Kwani mpo wangapi mnaoathitika na hayo maji niangalie uwezekano?
 
Unajua hali ya rufiji ni kama vile inafichwa fichwa ila ukitizama picha ya mafuriko unaona kuna uwezekano, hayo maeneo ndiyo basi tena watu kuishi hata baada ya mradi kukamilika kwa sababu hali hii itakuwa ni ya mwendelezo kila msimu wa mvua ambapo maji yatakuwa yanafunguliwa yakijaa bwawani, au yatakuwa hayajai?

Cha kufanya, serikali isitake kukwepa wajib na kuleta janja janja, mfano wasianze kusema "wakazi ndio walifuata njia ya maji" wakati kabla ya bwawa walikuwa wanaishi tu".Ingawa nahisi serikali haitawatelekeza raia wa rufiji.

Serikali iwalipe fidia waathirika na wahame hayo maeneo kama hayafai kuishi tena.

Kama serikali iliweza kuwahamisha Wamasai Ngorongoro na kuwajengea nyumba + pesa taslimu, kwa nini washindwe kuwahamisha wakazi wa rufiji katika hizo kata zilizoathirika kama hazifai tena kuishi watu?
 
Back
Top Bottom