TANESCO sitisheni kampeni ya TUNAJIPANGA, watu wanachotaka ni kupata umeme

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Wiki ijayo jumatatu terehe 29/11, Tanesco watakua na kampeni ya TUNAJIPANGA.

Lengo ikiwa ni kutambua changamoto ambazo wananchi wanazipata kwenye umeme.

Hili naliona ni suala la ajabu, sasa hivi kuna shida kubwa sana ya umeme Tanesco yapaswa wajikite kutatua changamoto hizi za umeme kuliko kuja na hizi kampeni.

Fanyeni juu chini tupate umeme, hayo makampuni hayasaidii kitu.

Sijui ni kina nani wanakuja na mawazo ya aina hii, inastaajabisha na kusikitisha.

20211122_221355.jpg
 
Wiki ijayo jumatatu terehe 29/11, Tanesco watakua na kampeni ya TUNAJIPANGA.
Lengo ikiwa ni kutambua changamoto ambazo wananchi wanazipata kwenye umeme.
Hili naliona ni suala la ajabu, Sasa hivi Kuna shida kubwa sana ya umeme Tanesco yapaswa wajikite kutatua changamoto hizi za umeme kuliko kuja na hizi kampeni.
Fanyeni juu chini tupate umeme, hayo makampuni hayasaidii kitu.
Sijui ni kina nani wanakuja na mawazo ya aina hii, inastaajabisha na kusikitisha.
View attachment 2020566
Wanajipanga na Christmas hela ya kutanulia😅
 
Haya ni matokeo ya uongo wa JPM.
Mnyonge mnyongeni. Haki yake mpeni. Enzi za JPM usingeweza kuona mazingaombwe yote yaliyoanza kuonekana awamu hii. Haya masijui Tunajipanga,mara makamba kuruka na chopa. Enzi za JPM tulishaanza kusahau habari za umeme kukatika,maji kukatika. Siku hizi umeme unakatwa saa 1 asubuhi mpaka saa 5 usiku ndio unarudishwa. Enzi zake usingeona hicho kitu
 
Tulidanganywa tuna ziada ya MW 350 hivi, leo tunaambiwa ukame umesababisha upungufu wa MW 200 hivi, sasa kwa mahesabu rahisi tusingekuwa na upungufu kwani tulikuwa na ziada. Leo hii inashangaza kuona tunaanza tena kuwasha majenereta ya DOWANS, SYMBION na wengine huku gesi yetu ikiwa haitumiki! Tuliambiwa tunauza umeme nje, kweli?!
 
Tatizo linaanzia kwa wananchi. Watz ni mazuzu sana ni waoga hatari. Huu umekuwa mradi wa watu wachache kujipigia pesa. Watu wengi wanajua,ila wanaogopa. Tutarudije kwenye mamiradi ya kifisadi ya Dowans?.

Nimeamini asilimia kubwa ni Magufuli tu aliiweza hii nchi. Vinginevyo mpaka CCM iondolewa madarakani ndio kuisha kwa huu uozo. Inasikitisha sana juzi tu Magufuli yupo tulishaanza kusahau habari za umeme kukatika. Nikauza mpaka na sorah yangu. Kweli tutamkumbuka. Hawa majitu yana roho mbaya
 
Kuna loop hole kubwa sana kwenye uongozi wa nchi kwa sasa, huko mawizarani na kwenye taasisi za serikali watu wanajiachia tu, na bahati nzuri wapigaji wamewekwa jikoni no way, muhimu watuambie huko "KUJIPANGA" watatumia how much.
 
Back
Top Bottom