Tanesco Tabata Mnashirikiana na Wezi. Hili tumelifahamu msibishe!

Tanesco Tabata Mnashirikiana na Wezi. Hili tumelifahamu msibishe!

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Tabata hasa huku maeneo ya Chuoni St. Marys, Camp, Bima n.k Mmekuwa mnakata umeme usiku ili wezi watuibie kila mara.

Leo mlikata tena wezi wakaruka ukuta ndani kumbe mimi sijalala. Hiii kesi wengi wanasema ni Ushirikiano mwema wa TANESCO na Wezi. Mnakata bila sababu za msingi kila siku usiku na kurudisha usiku wa manane au saa sita tayari watu wakiwa wameshaibiwa.

Huu mchezo ni wa hovyo. Sababu za kukata umeme ni nini Nyie watu? Mbona hamsemi? Haya mnayafanya sana kipindi hiki sababu mnajua hakuna wa kuwafokea. Why eneo letu tu kila mara umeme ukatwe? Kesho yake tunakuja sikia watu wameibiwa TV n.k?

Msibishe, mtaniudhi. Msibishe sababu ndo ukweli ulivyo ulizeni mtaambiwa na wenyeji maeneo hayo.
 
Mkuu saa sita usiku inakuwa unaita ni usiku wa manane? Unalala saa moja jioni nini?

Anyway poleni
 
Back
Top Bottom