DOKEZO TANESCO Tarime siyo waadilifu, bila kutoa rushwa huunganishiwi umeme kwa wakati

DOKEZO TANESCO Tarime siyo waadilifu, bila kutoa rushwa huunganishiwi umeme kwa wakati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
TANESCO wilaya ya Tarime wamekuwa siyo waadilifu kutekeleza majukumu yao, inashangaza wateja wanalipia toka mwezi wa pili mwaka 2024 mpaka mwezi huu wa nane hawajaunganishiwa umeme!

Ukienda ofisini kuuliza wanakwambia nguzo hazipo ama vifaa vyako havijafika huku wengine wanalipia na wanaunganishiwa umeme ndani ya wiki (kwa rushwa...Kama ni uongo mifumo inazungumza)

Naomba mamlaka husika iliangalie hili, vinginevyo wataendelea kuichafua Serikali yetu pendwa.
 
Baadhi ya Huduma za serikali bila chochote kitu watakuchelewesha sana
 
Bhiita ni biitha murah.
Kwani huna panga?
 
TANESCO ya Tabata Liwiti ndio balaa, unaweza kaa miezi mitatu baada kulipia na haupati huduma, ukienda kwenye kile kikontena chao ni kama kijiwe cha wavuta bangi, vululu, hata haieleweki nani ni nani na ana majukumu gani, wanarushiana mpira tu
 
Back
Top Bottom