TANESCO: Umeme kukatika usiku (Disemba 18, 2024) ni hitilafu katika gridi ya taifa

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Pale ambapo taarifa inakuja zaidi ya saa baada ya umeme kukata! Walikuwa wanasikilizia kwanza kuona muujiza ama? Nyinyi TANESCO na DAWASA Wizara ya Maji siku hizi hamna maana kabisa.

Mbu kwa kushirikiana na joto, usiku utakuwa mrefu kweli leo!

======

TANESCO wamesema kuwa kukatika kwa umeme usiku wa leo Jumatano Desemba 18, 2024 kumesababishwa na hitilafu katika gridi ya Taifa.

"Shirika linautaarifu umma kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika Mfumo wa Gridi ya Taifa leo tarehe Desemba 18, 2024 majira ya saa 06:12 Usiku hitilafu hiyo imepelekea Mikoa inayopata umeme katika Gridi ya Taifa kukosa umeme.

"Timu ya wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme katika maeneo yote yanayokosa huduma ya umeme."

1734477796739.png
 
Hii nchi tunafanya mambo kienyeji sana. Hivi wafanyabiashara wanafidiwa vipi hasara wanayoipata kutokana na kukatika kwa umeme?

Mtu amenunua umeme wa kutosha, ametimiza wajibu wake lakini shirika linaposhindwa kutimiza wajibu wake kuhakikisha mteja anapata huduma linawajibika vipi?
 
Huku Dodoma umerudi dk 5 zilizopita.
Tunasikilizia kama utakata tena ⏱️
 
Wakuu,

Pale ambapo taarifa inakuja zaidi ya saa baada ya umeme kukata! Walikuwa wanasikilizia kwanza kuona muujiza ama? Nyinyi TANESCO na DAWASA Wizara ya Maji siku hizi hamna maana kabisa.

Mbu kwa kushirikiana na joto, usiku utakuwa mrefu kweli leo!

======

TANESCO wamesema kuwa kukatika kwa umeme usiku wa leo Jumatano Desemba 18, 2024 kumesababishwa na hitilafu katika gridi ya Taifa.

"Shirika linautaarifu umma kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika Mfumo wa Gridi ya Taifa leo tarehe Desemba 18, 2024 majira ya saa 06:12 Usiku hitilafu hiyo imepelekea Mikoa inayopata umeme katika Gridi ya Taifa kukosa umeme.

"Timu ya wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme katika maeneo yote yanayokosa huduma ya umeme."

Kwa hii kasi ya kukatika katika umeme,tunaanza kurudi kwa kasi sana miaka ya 2000

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni kwamba watanzania tunachezewa sana na umbwa wachache wanaojiona hii nchi ni ya baba yao. Anyway siku yaja tu hata kama ni miaka 30 ijayo lakini hiyo siku ikifika wakimbir wakafiche matumbotumbo yao huko vichakani..
 
Punguza ukali wa maneno, mkuu. Wala huhitaji kutukana ili pointi yako ieleweke.
 
JNHPP ni Useless umeme kila siku kukatika halafu visababishi ni minor issue ambazo zinaonyesha maintance hawafanyi ,ningekuwa mimi ni waziri ningefukuza operation managers wote.
 
Back
Top Bottom