Tanesco wa Ziwa Tanganyika

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Leo kwenye pitapita zangu nikakutana na huyu mwamba! Jina lake limenipotea ila nimepata kusikia watu wakimuita TANESCO wa Ziwa Tanganyika.

Wanadai anachezesha shoti za umeme hatari! Je ni kweli kuwa huyu samaki sio wa kumgusa ovyo kama unavyomgusa Sato ama Sangara?
 
Ni kweli ziwa Tanganyika wamo samaki wanaojilinda kwa kutoa umeme, samaki wa aina hii hata baharini wamo na wanatoa umeme unaoweza kuwasha taa ya voti 120 na kuendelea. Chukua tahadhari kaa mbali naye.
 
Ila si analika vizuri sana
 
Ni kweli ziwa Tanganyika wamo samaki wanaojilinda kwa kutoa umeme, samaki wa aina hii hata baharini wamo na wanatoa umeme unaoweza kuwasha taa ya voti 120 na kuendelea. Chukua tahadhari kaa mbali naye.
Kumlaz ni zaidi ya volts350+. Yaani mara 3 ya umeme wa nyumbani wa kuwasha tv la chogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…