TANESCO wakata umeme mbele ya Mkutano wa Rais, Kilimanjaro

TANESCO wakata umeme mbele ya Mkutano wa Rais, Kilimanjaro

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Hali hii ya sintofahamu ilitokea siku ya leo katika ukumbi wa Kuringe Moshi, Ambapo Umeme ulikatika ghafla na kuleta taharuki ya kiusalama Ukumbini.

Ni Vyema Uongozi wa juu wa TANESCO uwe unafanya maandalizi ya ukarabati na kuhakikisha umeme unakuwepo wakati wote pindi Kiongozi Mkuu wa Serikali anapokuwepo mkoa husika

Matatizo ya kukatika Kwa umeme yameendelea kuathiri uchumi wa TANZANIA
 
Hali hii ya sintofahamu ilitokea siku ya Leo katika ukumbi wa Kuringe Moshi, Ambapo Umeme ulikatika ghafla na kuleta taharuki ya kiusalama Ukumbini.

Ni Vyema Uongozi wa juu wa TANESCO uwe unafanya maandalizi ya ukarabati na kuhakikisha umeme unakuwepo wakati wote pindi Kiongozi Mkuu wa Serikali anapokuwepo mkoa husika,
Matatizo ya kukatika Kwa umeme yameendelea kuathiri uchumi wa TANZANIA ,
Wacha wakate
 
Kazi nzuri Tanesco, si wamepanga kuchukua 11trillion, kateni tu bila kujali sura zao

Failed state, maandalizi ya uwepo wa Raisi wa nchi kisha umeme unakata, kweli?
 
Hali hii ya sintofahamu ilitokea siku ya leo katika ukumbi wa Kuringe Moshi, Ambapo Umeme ulikatika ghafla na kuleta taharuki ya kiusalama Ukumbini.

Ni Vyema Uongozi wa juu wa TANESCO uwe unafanya maandalizi ya ukarabati na kuhakikisha umeme unakuwepo wakati wote pindi Kiongozi Mkuu wa Serikali anapokuwepo mkoa husika

Matatizo ya kukatika Kwa umeme yameendelea kuathiri uchumi wa TANZANIA
Kigoma meneja alitumbuliwa baada ya umeme kukatika mbele ya Rais. Hata hapo Moshi Meneja ajiandae kutumbuliwa usiku huu.
 
Kazi nzuri Tanesco, si wamepanga kuchukua 11trillion, kateni tu bila kujali sura zao

Failed state, maandalizi ya uwepo wa Raisi wa nchi kisha umeme unakata, kweli?

Kwamba wakikata ndio haito tumika? Feel sorry for you man
 
Hii nchi achukue Elon Musk tu ndo maisha yatakua rahisi. Ndo mana TANESCO na TCRA wanamuogopa huyu jamaa maana hela ambazo walikua wakizichuja na kusingizia wanakata umeme kisa maji yamepungua, zitakua zinaenda kihalali
 
Mi nadhani achukue Putin
 
Mi nadhani achukue Putin
Tena Putin akichukua ndo maisha yatakua bata hatare. Madini yote tutayapeleka kwake na sisi tutapata umeme ambao haukatiki na mabando nafuu kama yote. Ajira zitakuwepo kama zote maana miundombinu atahitaji kuiboresha kama nchi yake. Yule jamaa ni mtu mwenye roho nzuri sana watu wahajui tu.

Iyo nchi wanaojifanya kumpiga eti kisa kipande fulani ni cha kwao, kama angetaka kuwapiga si angewaangamiza tu chap.

Utasikia mtu anasema eti Putin hawezi kuwaangamiza kisa anaogopa aftermath ya nchi kama America na UN, ni uongo. Hawaogopi wala nini. Ni huruma tu anayoonyesha kwa watu wengine ambao hawana mpango wa kuhusika na vita vya kipumbavu but since wanaweza wakaget involved ndio maana anaonyesha huruma.

Unadhan angekua na roho mbaya kama mjamaa wetu wa North Korea si angeifuta iyo nchi duniani afu akapambana na hiyo aftermath ambayo in the end haiwez kurudisha uhai wa waliokufa?
 
Back
Top Bottom