TANESCO wameigomea bei elekezi ya Tsh 27,000

Alisema"mtanikumbuka kwa mema"! Hao wafanyakazi wa Tanesco wanaoweka mgomo baridi kwa nini wasitimuliwe wote iwe fundisho kwa wengine! Wakirudi mtaani na wao wawe wanapanga foleni ya kuunganishiwa umeme ili wajifunze! Dr. JPM, we really miss you! May your precious soul rest in eternal peace and power our great African hero, amen 🙏!
 
Mwaka Jana wakati nataka vuta umeme kwangu nilijifunza jambo. Maagizo ya waziri hayana barua/ waraka na pia si kila eneo wanaweka kwa 27000. Inategemea kama mahali ulipo kuna miradi/ programu ya kuweka umeme kwa 27000. Pia nilijifunza, 27000 ni kwa eneo lisilohitaji nguzo ie kuna nguzo karibu wewe ni kufungiwa mita tu na kuingiza ndani.

Maagizo ya waziri yanawatesa sana mameneja wa TANESCO wa Wilayani. Inatakiwa afafanue 27000 ni kwa kigezo kipi na sio kubwatuka tu.
 
Gharama halisi sio hiyo 27,000, nani analipia hela inayobaki?

Serikali kama imeamua kuwapa watu umeme kwa bei wanayotaka wafanye hivi

1. Mtu akaombe gharama halisi kwa TANESCO
2. Apeleke makadirio kwa Waziri na hiyo 27,000 yake
3. Serikali ilipe Tanesco 27,000 + gharama za juu.

Case closed
 
Malipo ya 27,000 yanalipwa kwenye nyumba yenye sifa ambayo ipo ndani ya mita 30,
Nyumba yako ikiwa mbali zaidi ya mita 30 na panahitaji nguzo inabidi usubirie mpaka Tenesco walete miundombinu yao Nguzo na waya ziwe karibu ndani ya mita 30 utalipa hiyo elf 27.

kama Nyumba yako iko mbali zaidi ya mita 30 sehemu yenyewe Nguzo basi tambuwa kuwa hauna vigezo na sifa ya Kulipa 27,000
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Mimi mliniomba taarifa za nyumba yangu nikawapatia kila taarifa mlioitaka inbox PM ila hamjanijibu ni wiki ya pili hii na wala sioni matumaini ya kuungiwa umeme ni mwezi unaenda wa tatu huu pamoja na kuwa nimeishalipia 690,000/= TANESCO TANESCO
 
Huyu kukujibu lazima akuombe vyote au kimojawapo ya vifuatavyo
1. Uende PM
2. Umpe meter number
3. Utaje jina lako

Yaani utafikiri bila kumpa hayo makitu hatakumbuka majibu vizuri..
Binafsi huwa nafikiri huwa tunachat na robot, haimakini kwa mtu anayetafuta kuunganishiwa umeme halafu awe na hiyo meter number tayari
 
Control number Tanesco ni jibu toka kipindi cha Magu. Wakati taasisi nyingine mteja anatengeneza control number mwenyewe, Tanesco wao lazima wakutengenezee. Ukiomba wakutengenezee wanadai mtandao unasumbua. Ila ukiwatumia vishoka ndani ya dakika kumi unakuwa na control number tayari. Serikali itakayoweza kuwadhibiti Tanesco itakuwa serikali iliyofanikiwa sana, zingatia hata Magu kawashindwa.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Hapo kwenye kuliwa na mchwa mzee umezidisha chumvi ingawa ni kweli Kuna urasimu sana
Hata mimi naziona sana nguzo zimesahaulika hadi kuliwa na mchwa! Lakini ukitaka huduma unaambiwa hakuna nguzo! Kama kuna kiongozi haamini aweke simu yake hapa tuwe tunamjulisha nguzo zilizosahaulika/kuliwa na mchwa. Halafu huwa inatokea wakimaliza kazi huenda kupitisha umeme maporini nguzo zinazobaki huwa zinaachwa huko2 hata ukienda baada ya miaka 10 utazikuta. Yaani hiyo ni kawaida sana kwa tanesco. Hawana uchungu maana ni mali ya umma. Nashauri viongozi wanaowekwa kusimamia mashirika ya umma nyeti kama haya wawe wazalendo kweli2.
 
Kilaza kumbe wewe, kipi ambacho kinaishi milele?? Hata Chuma hakiishi milele
Matusi ni dalili za kukosa hoja... Kama haziishi milele, basi huwa zinaharibika..!! Be it kwa mchwa au chochote...!! that is where the point is..
 

Hiyo ni Dodoma aliko Waziri, hali ni mbaya zaidi huku mikoa mingine
Mkuranga pwani ni zaidi ya matatizo.
Unajaza fomu lakini saveya kuja kwako bila maalifa ni ndoto. Hiyo ni savey, kuungwa ni Jambo jingine. Watu wanamaliza miezi bila kutembele, ukipiga simu unajisumbua. Meneja ndo hapokeagi simu kabisa labda za wakezake.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM

Kwani katika huu uzi nini hamjaelewa hadi uombe hizo detail?
Uzi upo wazi mnataka jina la kazi gani...!?
Nguzo zenu huko zinaliwa na mchwa aisee..
 
Kwani katika huu uzi nini hamjaelewa hadi uombe hizo detail?
Uzi upo wazi mnataka jina la kazi gani...!?
Nguzo zenu huko zinaliwa na mchwa aisee..
Tuma taarifa hata inbox ( PM)ili tukuhudumie
 
Kwa desturi za watanzania, hapo ni kutengeza ugomvi hata Kama kisemwacho kipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…