TANESCO wamejipanga kupata hasara ya Tsh. Trilioni 13.34 kwa miaka mitano ijayo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mahitaji ya umeme yataongezeka hadi kufikia megawatts 4,000 mwaka 2025 huku uwezo wa TANESCO ukiwa ni kuzalisha megwatts 1,600 kukiwa na tofauti ya Megawatts 2,400 ambayo ni Upungufu wa 60%.

WAkati huo mradi wa Mwalimu Nyerere uliotarajia kuzalisha Megawatts 2,115 ukiwa ni kizungumkuti kutokana na kukumbana na cha ngamoto ya mabadiliko ya tabia nchi , hali inayoleta mashaka kwa Tanzania kuwa na uwezekano wa kukumbana na uhaba mkali wa nishati ya umeme kwa miaka minne ijayo.

KAtika mpango mkakati wa miaka mitano ijayo TANESCO wamejipanga kutumia Tsh. Trilioni 26.17 ili kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme. Gharama hizi zinawasilisha hasara ya Tsh. Trilioni 13. 34 kwa kuwa jumla ya mapato wanayokadiria kukusanya kwa miaka mitano ni Tsh. Trilioni 12.83.

1637646807200.png

Hasara inaweza kuwa kubwa zaidi kwa kuwa haijaweka gharama za uendeshaji za kila siku kama malipo ya mishahara, nishati ya maji nk, kwa kuwa hela iliyotajwa hapo ni ya kuongeza uzalishaji wa umeme tu!

TANESCO wamejipanga kupata mapato ya Trilioni 1.9 kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo katika mpango mkakati wa TANESCO wanatarajia kuongeza mapato kila mwaka wa fedha. Mwaka 2021/22 wamepanga kupata mapato ya Tsh. Trilioni 2.

Katika mpango Mkakati wa 2021/22 hadi 2025/26 TANESCO itakuwa imefanikiwa kuongeza mapato kwa 25% ambapo mwaka 2025/26 watakusanya Tsh. Trilioni 2.39.
 
Hii nchi ina matatizo mengi mno, na kisababishi kikubwa ni mambo ya siasa za kinafiki, siasa zetu zinaimaliza nchi hii, haiwezekani miaka 60 ya Uhuru tushindwe hata kumaliza tatizo moja kubwa la kujivunia - tuna matatizo makubwa mno yanatukabili leo.

Elimu - tumeshidwa kabisa
Maji - hamna kitu
Nishati hasa Umeme - matatizo kama hivi mnavyoyaona.
Afya - huko ndiko ni balaa

Ni kipi ndugu zangu watanzania mtajivunia ndani ya hii miaka 60 ya uhuru wetu kwamba mmekifanya vizuri na mfano wa mataifa mengine? Siasa zetu za kishabiki zinalighalimu hili taifa.
 
Mahitaji ya umeme yataongezeka hadi kufikia megawatts 4,000 mwaka 2025 huku uwezo wa TANESCO ukiwa ni kuzalisha megwatts 1,600 kukiwa na tofauti ya Megawatts 2,400 ambayo ni Upungufu wa 60%.

WAkati huo mradi wa Mwalimu Nyerere uliotarajia kuzalisha Megawatts 2,115 ukiwa ni kizungumkuti kutokana na kukumbana na cha ngamoto ya mabadiliko ya tabia nchi , hali inayoleta mashaka kwa Tanzania kuwa na uwezekano wa kukumbana na uhaba mkali wa nishati ya umeme kwa miaka minne ijayo.

KAtika mpango mkakati wa miaka mitano ijayo TANESCO wamejipanga kutumia Tsh. Trilioni 26.17 ili kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme. Gharama hizi zinawasilisha hasara ya Tsh. Trilioni 13. 34 kwa kuwa jumla ya mapato wanayokadiria kukusanya kwa miaka mitano ni Tsh. Trilioni 12.83.

View attachment 2020486

Hasara inaweza kuwa kubwa zaidi kwa kuwa haijaweka gharama za uendeshaji za kila siku kama malipo ya mishahara, nishati ya maji nk, kwa kuwa hela iliyotajwa hapo ni ya kuongeza uzalishaji wa umeme tu!

TANESCO wamejipanga kupata mapato ya Trilioni 1.9 kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo katika mpango mkakati wa TANESCO wanatarajia kuongeza mapato kila mwaka wa fedha. Mwaka 2021/22 wamepanga kupata mapato ya Tsh. Trilioni 2.

Katika mpango Mkakati wa 2021/22 hadi 2025/26 TANESCO itakuwa imefanikiwa kuongeza mapato kwa 25% ambapo mwaka 2025/26 watakusanya Tsh. Trilioni 2.39.

4D7000B7-04CC-41DB-85E0-295935C62B69.jpeg
 
Back
Top Bottom