Wanajamvi nina kijana wangu alifanya interview ya kazi TANESCO, kama kawaida majibu yanafuata bgaadae. Baada ya wiki mbili kijana wangu alitumiwa barua iliyosainiwa na meneja wa Tanesco ikimpa hongera zake amefaulu interview na kumwaarifu kuwa asubiri pindi taratibu za ajira zitakapokamilika ataitwa akasaini mkataba.
Hiyo ilikuwa ni June, sasa mpaka leo hawa jamaa wako kimya na huyu kijana nikimwambia afanye application sehemu nyingine anakataa eti tayari ana baru ya TANESCO kwamba tayari ni mfanyakazi wao. Naombeni wadau sheria inasemaje juu ya jambo hilo? mwanangu asikae tu anasubiri ajira kumbe hakuna.