TANESCO wameturudisha nyuma miaka 10 umeme kukatika mara 5 Kwa siku

TANESCO wameturudisha nyuma miaka 10 umeme kukatika mara 5 Kwa siku

live on

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
855
Reaction score
1,365
Haya mambo tulisha yasahau Baada ya Magufuli kuingia madarakani alikomesha kabisa haya mambo
Kama umeme ulikatika basi ni Kwa sababu za msingi na taarifa ilitokewa

Lakini hili linaloendelea Kwa Sasa umeme kukatika mara 5 Kila siku bila ya sababu zozote za msingi tulisha yasahau haya

Kama ni mgao wa masaa mawili mawili au matatu Kwa Nini hamtoi taarifa?

Kama ni ubovu wa Transformer kwanini msitengeneze miezi yote hiyo?

Alafu Magufuli alipokuwa anakutumbueni mkawa mnasema hafati haki za wafanyakazi

Ukweli ni kwamba hi nchi bila ya kutumbua tumbua mambo hayaemdi

Hapa unaweza kukuta hata meneja wa Tanesco mkoa wa Temeke hajui kama huku Chamazi umeme Kila siku unakatika mara 5 au 6 na hakuna taarifa yoyote

Sasa meneja kama huyo kwanini asitumbuliwe?

Hapa sahizi umeme hakuna Sasa sijui Kuna nguzo imeanguka au Transformer imelipuka

R.I.P Jembe langu
 
Back
Top Bottom