KERO TANESCO wanakata umeme karibu Mara 30 kwa siku huku Yombo Vituka

KERO TANESCO wanakata umeme karibu Mara 30 kwa siku huku Yombo Vituka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mfugaji123

New Member
Joined
Apr 3, 2020
Posts
4
Reaction score
42
Katika hali isiyo ya kawaida kumekuwa na tatizo la mara mara la kukatika umeme katika maeneo ya Yombo Vituka, jijini Dar Es Salaam.

Kwa siku umeme unaweza kukatika hata mara 30 . Umeme ndani ya saa 1 unaweza kukatika hata mara 5. Hali hii imesababisha kukwama kwa shughuli nyingi za kiuchumi zinazotegemea umeme.

Pia huhatarisha usalama wa vyombo wa umeme katika sehemu za kazi na majumbani.

Taarifa kutoka TANESCO walipoulizwa walijibu majibu ya kawaida eti umeme hukatika kama unavyoweza kukatika sehemu zingine kukiwa na tatizo la ufundi au marekebisho ya miundombinu.

Lakini ukweli ni kwamba umeme huku Yombo ni kama mwanga wa kibatari dakika mbili upo dakika 2 hakuna. Kwa Kweli hii ni kero kubwa.

Umeme hauminiki hapa Yombo Vituka!!
 
Back
Top Bottom