Tanesco waomba radhi kukatika kwa Umeme gridi ya Taifa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa rasmi ya hitilafu kubwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa, iliyotokea majira ya saa 2:36 asubuhi na kusababisha kukatika kwa huduma ya umeme katika mikoa yote inayounganishwa na gridi hiyo.

Kwa mujibu wa TANESCO, timu ya wataalamu inaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu ili kubaini chanzo halisi cha hitilafu hiyo na kuhakikisha huduma ya umeme inarejea

Treni ya abiria ya SGR iliyokuwa ikitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam leo asubuhi imekwama katika eneo la Stesheni ya Pugu.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kukwama kwa treni hiyo kumesababishwa na hitilafu kwenye Gridi ya Taifa iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya umeme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…