TANESCO watufahamishe umeme tuutarajie lini

TANESCO watufahamishe umeme tuutarajie lini

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Huu ni uhuni kama ulivyo mwingine tu. Mambo haya hayakutokea nchi chini ya JPM.

Hivi sasa nchi yote kasoro visiwani Iko gizani.

Usalama wetu majumbani, vilivyoko kwenye majokofu, uzalishaji mali wenye kutegemea umeme, Simu zetu kuwasiliana na wapendwa nk nani anawajibika.

Hii haikubaliki Kwa hakika TANESCO waseme umeme tutegemee lini vinginevyo kuwaburuza wahuni hawa mahakamani hakuwezi kuwa muhani.

Ikumbukwe luku tumelipia, pesa zetu wanazo na kinyume cha makubaliano umeme hawatupi na wametulia tuliii!
 
Kwani Ndugu hujui mfumo wetu wa manunuzi,kama kuna chakuagizwa kwa ajili ya kutatua tatizo,bila miezi sita, mwaka ikitokea kwa uchache miezi 3,tuagize tutengeneze we kwa kujibu wa mikataba yetu mingi ya mchongo😂😂😂🤸🤸🤸
 
Kwani Ndugu hujui mfumo wetu wa manunuzi,kama kuna chakuagizwa kwa ajili ya kutatua tatizo,bila miezi sita,mwaka ikitokea kwa uchache miezi 3,tuagize tutengeneze we kwa kujibu wa mikataba yetu mingi ya mchongo😂😂😂🤸🤸🤸
JPM akiwa kazini vitabia hivyo viliondoka. Kama ndivyo hili lisimwache kigogo ofisini. Ofisini kigogo atakuwa anafanya Nini wakati mwenyewe kasema kachoka kuendelea na safari?
 
Acha kulia lia

Umeme upo kabla ya Tanesco

Tanesco imeanzishwa 1964 lakin Franclin kagundua Umeme tangu 1700s

Ukiona Tanesco wakikata umeme huna plan B ya kuwa na Umeme achana na heka heka za Katiba mpya sijui Mkataba wa Bandari pigania kwanza maisha yako na familia yako
 
Ile hali ya kuoga gizani Mara moja kwa wiki inajirudia tena?

Wakati ule maji na umeme ulikuwa unakatika kila siku.

Mmatumbi kalaaniwa kweli.

14729.png
 
Acha kulia lia

Umeme upo kabla ya Tanesco

Tanesco imeanzishwa 1964 lakin Franclin kagundua Umeme tangu 1700s

Ukiona Tanesco wakikata umeme huna plan B ya kuwa na Umeme achana na heka heka za Katiba mpya sijui Mkataba wa Bandari pigania kwanza maisha yako na familia yako

Plan B ya kuwasha jokofu wewe unayo?

Usiige kunya Kwa tembo wa masaki mjomba ..
 
Back
Top Bottom