TANESCO yaomba radhi wateja wake kwa kukatika kwa umeme ghafla usiku leo 21.01.2022

TANESCO yaomba radhi wateja wake kwa kukatika kwa umeme ghafla usiku leo 21.01.2022

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari,

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Wa Kinondoni Kusini limewaomba radhi wateja wake wanaotumia laini za umeme kwa kukosa huduma ya umeme muda huu.

"Maeneo yaliyoathirika ni Magomeni, Mburahati, Kigogo, Mabibo, Sinza, Ubungo,Bonyokwa, Kimara Baruti, Korogwe, King'ongo, Kimara Mwisho, Suca,Kwembe, Temboni,Maeneo ya Mbezi, Maeneo ya Kibamba, Makabe, Msumi, Msakuzi, Mpigi mageo, Malamba mwili, Kingazi, Makongo, Saranga, Changanyikeni, Chuo Kikuu na Mandela Road"

"Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kuweza kuhakikisha hali ya huduma ya umeme inarejea kwa wakati, Ndugu wapendwa wateja wetu, tunaomba uvumilivu wenu katika kipindi hiki cha kukosekana kwa huduma, Shirika linaomba sana radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza katika kipindi mnachokosa huduma ya umeme"

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Umeme wa Tanzania una allergy na mvua.
... ni jambo la kushangaza sana! Yakianza manyunyu tu probability ya umeme kukatika ni 100% wakati ndio muda ambao umeme unahitajika zaidi. Eti nyie jamaa TANESCO mna matatizo gani yasiyoisha miaka na miaka? Au ndio akili zile zile zinapewa jukumu la kuondoa matatizo zilizoyasababisha zenyewe?
 
Back
Top Bottom