TANESCO yashitukia mkataba wa Songas

TANESCO yashitukia mkataba wa Songas

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
Tuesday, 24 May 2011 20:08 newsroom


NA MOHAMMED ISSA

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema mkataba kati yake na kampuni ya gesi ya Songas una utata na unaweza kulisababishia hasara kubwa. TANESCO imesema mitambo ya Songas haiwezi kuzalisha megawati 160 kwa sasa, kwa kuwa haina uwezo wa kutumia gesi na mafuta kuiendesha. Kwa mujibu wa TANESCO, inahitaji sh. trilioni 1.3 kwa ajili ya marekebisho ya mitambo na imekuwa ikipoteza sh. bilioni 51 kwa mwaka kwenye mikoa ambayo haijaunganishwa na gridi ya taifa. Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi William Mhando, alisema hayo jana katika ofisi ndogo za Bunge, mjini Dar es Salaam, mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Mhando alisema mkataba wa Songas ni lazima uangaliwe upya kabla haujaleta madhara. Alisema kampuni ya Pan Africa ambayo hivi sasa imezima mitambo yake kwa ajili ya kuifanyia marekebisho makubwa imekiuka mkataba. Kwa mujibu wa Mhando, kampuni hiyo inapaswa kuzima mitambo kila baada ya miaka minne lakini imekaa hadi miaka saba haijafanya ukarabati.
aseven.jpg



Alisema kuzimwa kwa mitambo hiyo kumeongeza makali ya mgawo wa umeme, ambapo hivi sasa ni saa 16 badala ya saa tano. Mhando alisema hali ya upatikanaji umeme bado itakuwa ngumu, na makali ya mgawo yanaweza kuongezeka hadi Julai, mwaka huu. Hata hivyo, alisema hatua kadhaa zimechukuliwa kwa ajili ya mchakato wa ukodishaji mitambo ya megawati 260. Alisema zabuni imeshatangazwa na kampuni 15 zimejitokeza, ambapo moja imekidhi vigezo vya kuzalisha megawati 70. Mtambo huo wa kukodi utafungwa Tanga, eneo la Majani Mapana. Mhando alisema TANESCO inaendelea kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha tatizo la umeme linapatiwa ufumbuzi, ambapo mazungumzo yanaendelea na kampuni ya Marekani kwa ajili ya kupata megawati 112. Naye Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema uzalishaji na ununuzi wa mitambo ya umeme iachiwe TANESCO bila ya kuingiliwa na serikali au wanasiasa. Alisema serikali inaendelea na juhudi za kulitafutia dawa tatizo la mgawo wa umeme, ambalo limekuwa gumzo nchini. Alisema wanaobeza dhamira hiyo ya serikali hawana nia njema na taifa.

Ngeleja alisema juhudi za makusudi zinafanyika kukamilisha dhamira ya serikali na wanatarajia kuongeza megawati 1,000 kwenye gridi ya taifa ifikapo mwakani. Akizungumzia upatikanaji umeme kwenye migodi nchini, Ngeleja alisema inatumia megawati 59.2 zinazozalishwa na gridi ya taifa. Waziri Ngeleja alisema wakati umefika kwa TANESCO kuangalia uwezekano wa kununua mitambo yake badala ya kukodi kwa gharama kubwa. Alisema serikali inaendelea kupokea maoni na ushauri wa Kamati ya Nishati na Madini kuhusu mustakabali wa TANESCO. Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti January Makamba, iliishauri TANESCO kuchukua hatua za makusudi kumaliza tatizo la umeme nchini. Wajumbe wa kamati hiyo waliwaomba wanasiasa kuacha kuzungumzia suala la DOWANS, badala yake waangalie uwezekano wa kuupatia ufumbuzi mgawo wa umeme.

Last Updated ( Tuesday, 24 May 2011 20:20 )
 
Naye Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema uzalishaji na ununuzi wa mitambo ya umeme iachiwe TANESCO bila ya kuingiliwa na serikali au wanasiasa. Alisema serikali inaendelea na juhudi za kulitafutia dawa tatizo la mgawo wa umeme, ambalo limekuwa gumzo nchini. Alisema wanaobeza dhamira hiyo ya serikali hawana nia njema na taifa.

haya si ndio mambo aliyosema IDRISSA RASHID akaambiwa wanasiasa kuingilia TANESCO muhimu
 
Unaweza kusema "umeshtukia" proposal ya mkataba, huwezi kushtukia mkataba ambao umeshaingia mkenge. Waandishi wetu mbona hawajaenda shule?

TANESCO inawezaje kusema mkataba wake na Songas una utata, sio wao wenyewe waliosaini mkataba?

Legal department ya TANESCO bado ina matatizo hata baada ya kum demote yule mama aliye preside wakati wa Dowans.
 
Unaweza kusema "umeshtukia" proposal ya mkataba, huwezi kushtukia mkataba ambao umeshaingia mkenge. Waandishi wetu mbona hawajaenda shule?

TANESCO inawezaje kusema mkataba wake na Songas una utata, sio wao wenyewe waliosaini mkataba?

Legal department ya TANESCO bado ina matatizo hata baada ya kum demote yule mama aliye preside wakati wa Dowans.


Taso hapo ni uelewa tuu mkuu wewe may be ni learned brother na unajua maana ya proposal na mkataba halisi
 
Back
Top Bottom