Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
MABORESHO YA MITA ZA LUKU KWA WATEJA WA TANESCO KANDA YA ZIWA NA KANDA YA MAGHARIBI
Jumatatu, 27 Mei 2024
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Simiyu, Tabora, Katavi na Shinyanga kuwa zoezi la maboresho ya mfumo wa LUKU litaanza kufanyika katika mikoa hiyo kuanzia tarehe 01 Juni 2024.
Lengo la mabadiliko haya ni kuendana na viwango vya mifumo ya LUKU vya kimataifa na kuongeza ufanisi wa mita za LUKU.
Mteja anaponunua umeme atapokea tarakimu kwenye makundi matatu, kila kundi likiwa na tarakimu ishirini. Mteja ataingiza tarakimu za kila kundi kwa mfuatano unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa simu (sms). Makundi mawili ya tarakimu yatakuwa kwa ajili ya maboresho na kundi moja la umeme ulionunuliwa.
Zoezi hili ni bure na litafanyika mara moja tu kwa mteja, baada ya kufanya hivyo mteja atakuwa amefanya mabadiliko hayo na ataendelea kupata kundi moja la tarakimu ishirini kila anapofanya manunuzi ya umeme.
Baada ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi zoezi litaendelea kwa mikoa mingine nchini kwa awamu tofauti, kadri Shirika litakavyotangaza kwa umma na mwisho wa zoezi hili nchini ni tarehe 24 Novemba 2024.
Kwa taarifa zaidi wateja wanaweza kuwasiliana nasi kupitia namba ya huduma kwa wateja 0748 550 000, namba za huduma kwa wateja kwa mikoa husika, namba ya WhatsApp 0748 550 000 au mitandao yetu ya kijamii.
Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA
TANESCO- MAKAO MAKUU
DODOMA