TANESCO yatangaza mgawo wa umeme


nitakutumia message baada ya masaa 3
 
Ifuatayo ni sehemu ya Hotuba ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kufungua Bunge mnamo 30 Disemba 2005 (zingatia suala la vipaumbele na mipangalio analolizungumzia Zitto):

Nishati

Mheshimiwa Spika:
Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vye umeme na nishati kwa ujumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani. Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini.

Mheshimiwa Spika:
Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo ndivyo tutakavyofanya. Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua mipango ya umeme wa mto Rusumo na Stigler's Gorge. Vile vile tutaharakisha upatikanaji wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.

Mheshimiwa Spika:
Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne ni kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa, kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma katika gridi ya Taifa.
 
kwa kweli hawa watu wa TANESCO lazima waondoke kwanza kabla ya kuanza kuongea nao chochote...wameshindwa kazi kabisa na hakuna excuse yeyote,na inavyoonekana umeme tatizo sio pesa hatuna ni uongozi mbovu tuu,they must go!
 
Its sad when even in the 21st century people can not get basic needs such as electricity on a daily basis. All we need is the basic.....leave aside all other luxuries and perks.....we just want the basics. Mama mjamzito aendee hospitali bila kuhofia kufa, watoto wapewe furksa za kwenda shule, maji umeme nk. Sasa hata hivi vina tushinda jamani?
 
Hii kampuni ya Noor Oil ina uhusiano wowote na huyu Al Noor hapo chini aliyeshughulikia suala la gesi ya Songo Songo kabla JK hajakabidhiwa mikoba ya suala hilo pale Wizara ya Nishati?

In ‘Africa's Winds of Change: Memoirs of an International Tanzanian', the former Minister responsible for Energy, Al Noor Kassum, documents how we ended up at the mercy of Dowans. I take the liberty to say so because it is a documentary of how we forfeited, nay, suspended an initiative that could provide us with a total capacity of 2,100 MW, 21 times more than the 100 MW from Dowans.

That initiative is what came to be known as the Stiegler's Gorge Power Project. The gorge is located on the Rufiji River. According to Kassum, in 1979 they proposed to use it to generate electricity. To that end Halfslund/Norplan of Norway were consulted to prepare a feasibility study for the project.

It is this study, financed by the Norwegian government, that showed the said grand capacity then thus spaced over four phases: "At the end of Phase I (1990-95) the capacity would be 300 MW; at the end of Phase II (1995-2005) it would be 900 MW; at the end of Phases III and IV (2005-15) it would be 2,1000 MW. Thus, the capacity could be stepped up as demand increased over time. This would also spread the total cost over a longer period."

Interestingly, these consultants estimated that the investment cost for all these phases would be USD 1,382 million - a mere two times the cost of Dowans' plant in non real terms. They also noted that it could meet all of Tanzania's projected power needs at least until 2010. Yes, indeed, until next year.

"Unfortunately", laments Kassum, "we were unable to obtain financing for the project." "Instead", he further laments, "the Mtera Dam was built for half the cost of Stiegler's Gorge project but supplied only 10 percent of the power that the other project would have made available."

His ‘in hindsight lamentations' doesn't end there. Tanesco, he laments nostalgically, "spent almost the same amount that the Stiegler's Gorge project would have cost on constructing many small power-generation plants that used fuel to produce electricity." So, after all, we didn't start thinking small now.

"Later", Kassum winds up his regrets, "Mwalimu Nyerere told me it had been a mistake not to go ahead with the Stiegler's Gorge project. Had the money spent on those power stations be used on the Stiegler's Gorge project, electricity could have been supplied through cables to the whole country and we would not have the frequent power shortages that continue to plague Tanzania today."

Full of hope, Kassum sums up by saying the "good news is that the current Government has announced its intention to revive the Stiegler's Gorge project". That was 2007. Today, two years later, in 2009, the scanty information we can gather from the meeting between Dr. Idris Rashidi and Hon. Zitto Kabwe's teams is that Stiegler's Gorge project among other projects have been delayed due to lack of funds etc.
 
Nikweli serikali inapaswa kuwajibika..na sasa ni zamu ya Rais kuwajibika. sio waziri mkuu tena....tatizo la nchi hii kwasasa ni maamuzi mazito hayafanyiki.kwasababu Rais anataka apendwe na kila tabaka matokeo yake kila tabaka linamlaumu....wengine watailaumu tanesco, lakini tulio karibu tunajua kuwa tatizo sio tanesco, sio kweli kwamba tanesco hawana mikakati, tanesco mikakati wanayo, tatizo ni serikali haitekelezi mikakati ya kitaalamu ya tanesco na hatimaye inabidi kila wakati tanesco walazimike kuchukua hatua za dharula....ni kwasababu mikakati ya muda mrefu haitekelezwi na serikali..
 

Hana uhusiano!
 
Piga chini Waziri na uongozi wote wa Tanesco..........damn!

Hapana Mkuu Ogah, hakuna wa kuwapiga chini hawa. Akiulizwa Mkuu pale Ikulu atasema "Najivunia rekodi ya shirika letu la TANESCO kusambaza umeme nchini. Hili la kukosa umeme ni matatizo ya Mwenyezi Mungu."

Ni uozo mtupu miaka nenda miaka rudi. Je, hizo $10.5 zilizonunulia jengo la ubalozi DC zingeelekezwa kununua mitambo ya kufua umeme Watanzania si tungefaidika zaidi!? Kweli kupanga ni kuchagua.
 
Mpaka naandika Muda huu tayari sehemu kubwa ya Dar kama sio nchi nzima ipo KIZANI tangu saa 1 na robo jioni hii... Mwenye taarifa please... Napatwa na wasiwasi kukiendelea kuwa na kiza hadi saa saba Nyumba nyingi zaweza kuungua kutokana na watu kusahau kuzima mishumaa na koroboi MASKINI WEEE!!!!!
 
Kwa jinsi hii siasa zetu zitaangamiza taifa letu.kwamba majuzi tulikataa kununua mitambo yenye mashaka kuwa ni ya watu wezi...dowans, leo nchi nzima imeingia giza...:
1.Wapo wanaosema atakumbukwa zitto kuhusu hili sio zitto peke yake, hata Ndesamburo alionya hili ndani ya tanzania daima j,pili wakati huo....Engineer stella manyanya alionya hatari ya siasa zetu katika hili alipohojiwa na gazeti la majira wakati huo...sijapata nukuu zao kwa haraka tu....lakini wabunge hawa waliweka msimamo wa kutaka nkununuliwa mitambo yenye uwezo tuweze kukabiliana na tatizo la umeme bila kujali mitambi hiyo ni ya nani....Blair ana msemo wa "change evil money into gud use"....

lakini nakumbuka wakati wa mjadala wa dowans, kuna wabunge walisema mitambo yenye uwezo wa zaidi ya ile ya dowans ingeweza kupatikana ndani ya wiki mbili tena kwa bei nafuu mara dufu kuliko hiyo ile ya dowans....sijui kama serikali au tanesco walipata msaada huo kutoka kwa wabunge,au wabunge hao waliweza kupeleka mapendekezo hayo serikalini......au zilikuwa siasa zetu za bongo za kujadili hoja with respect to aliyeitoa badala ya tatizo lenyewe.....kazi ipo!
 

.....why why why why?
 

...suala si ku-turn evil money into good use......suala hapa lilikuwa kulazimisha kufanya jambo evil wakati una nafasi ya kufanya jambo jema....na wala haikuwa kulazimisha politics........it was just a simple common sense............

Unaona mawasiliano ambayo Mh Zitto............. anaomba inf..........kutoka kwa memba wa JF Kokolo?..........hivi vitu si kwamba hakuna suluhisho kama watu walivyotaka tufikiri......watu wanalazimisha evil doings zao.....na sasa wanatukomoa kwa kuwa ufisadi wao tuliupigia kelele............

....ku-turn evil money into good use" ni kama vile pesa za EPA kutumika kwenye kilimo.....na sio kama suala la Dowans......you got it wrong.....my brother
 

Mkuu JM, they simply don't give a damn!
 

Ahsante sana Mkuu, uozo na matatizo mengi ya Serikali ya Kikwete unaanzia kwake mwenyewe ndiyo maana nimeshasema mara nyingi hastahili kabisa kugombea 2010. Hili la "CCM tuna utamaduni wetu wa kuachiana kiongozi akae madarakani kwa awamu mbili." Watanzania tulipige vita kwa nguvu zote.

Huyu mtu kishaonyesha hana uwezo wa kuiongoza nchi yetu kwanini ang'ang'anie kuendelea kuwepo madarakani pamoja na kuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kazi tuliyompa imemshinda!? Tunataka Rais mpya 2010 Kikwete hatufai kabisa Watanzania.
 

HII habari ni ya kweli,Mimi nilifanikiwa kuona utafiti wa baadhi ya wabunge kuhusu huu ufisadi,walikuwa na Dossier ya nguvu kuhusu hili na hizi taarifa zimeshaanza kufanyiwa kazi na wabunge kwa kuanzia tu Documents zote zimeshapelekwa kwa waziri mkuu kwa aushauri na kama hatachukua hatua November mtaliona hili Bungeni
 
Mimi nimesoma kwa makini maoni yote yaliyotolewa katika thread hii kuhusu tatizo hili la umeme. Kama nilivyotabiri katika mjadala huu ulipojitokeza awali kuhusu athari za wanasiasa kuingilia maamuzi ya kitaalamu ya kununua mitambo ya Dowans, nilisema kuwa utapotokea mgao wa umeme, ni wale wale waliopinga ushauri ule wa busara ndio hao hao watakuwa wakwanza kulaumu. Sasa naona watu wale wale wanatoa hoja zile zile walizozitoa wakati ule.

Mimi nilimuunga sana mkono Zitto kwa uamuzi wake wa kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans. Hivi sasa kaja tena na maelezo mazuri ya hali halisi ilivyo kuhusu nishati ya umeme badala tu ya kuilaumu Tanesco. Kama wananchi kweli wanataka Tanesco ifanye kazi yake sawasawa, basi Serikali iipe kazi mbili. Moja ya kuzalisha umeme na ya pili ya kutengeneza noti ili kila wanapotaka kununua mitambo au kujenga grid mpya basi wanazalisha noti za kiasi cha mahitaji yao. Hapo wakishindwa na mimi nitawalaumu.

Nitafurhi sana sasa katika hali hii tuliyofikia kumsikia Mh. Mwakyembe akitoa tena maoni yake kuwa ni bora nchi iingie gizani kuliko kununua mitambo ya Dowans. Ila safari hii kauli yake hiyo, ai back na tathmini ya faida na hasara zake kwa uchumi wa nchi kama alivyofanya Mh. Zitto. Asibane kimya tu au kuja na lawama zisizo na msingi za kuilaumu Tanesco.
 
ule mgao wa umeme uliokuwa ukisubiriwa rasmi naona umezonduliwa kwa ukamilifu leo hii;baadhi ya sehemu zimekuwa gizani kabisa..je ni kweli maji yamekuwa madogo ama kuna miradi ya watu ya majenereta wanataka kutupitishia kinguvu nguvu..kamamnakumbuka jamani ule mradi wa mama siti mwinyi ulivyopendeza kila mmoja akasema kweli kufa kufaana;;natumaini mama yangu kipenzi SALMA KIKWETE atokuwa kweye biashara hizi kama mzaziw mwenzetu aliekuwa akishusha makontena kwa makontena y jenereta kama alikuwa anaishi dubai.......
haya TANESCO tunawaombea kila la kheri sasa sijui ndio hasira za idrissa AMA
YOTE KHERI
 


Hata mtoto wa darasa la kwanza atajua kujumlisha na kutoa hizi hesabu. Ataweza pia kujua kwa mahesabu haya ingetuchukua miaka si zaidi ya miaka 5 kukopa, kujenga gridi mpya ya North-West na kulipa deni la 700mil usd. Leo hii kanda ya Ziwa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Mara ingekuwa na umeme wa uwahakika.

Tanzania imekosa viongozi makini...inasikitisha.
 

Sikubaliani na yeyote yule anayepigia au aliyepigia debe ununuzi wa mitambo ya Richmond/Dowans ambayo illingia nchini kifisadi.

Papa fisadi Rostam aliidanganya Serikali kwamba kampuni yake ina utaalamu wa kufua umeme na kampuni HQ yake ilikuwa iko Houston, Texas. Kumbe ni uwongo mtupu!

Alilipwa $200 millioni na TANESCO kati ya June 23, 2006 hadi August, 2008 pamoja na kutozalisha hata tone moja la umeme, huu ni wizi dhahiri.

Hakuna hata mtu katika Serikali anayefuatilia kwa Rostam ili kuhakikisha malipo ambayo alilipwa ambayo hayakuwa ya kihalali anayarudisha mabilioni hayo haraka iwezekanavyo Serikalini.

Hivyo kutaka kununua tena mitambo ile ambayo iliingia nchini kwa njia za kifisadi ni kama kuwatunuku mafisadi wale waliohusika na ufisadi ule ambao hawana popote pengine pa kuuza mtambo wao huo.

Kama tungekuwa na Serikali makini baada tu ya kufahamu kwamba kuna haja ya kununua mtambo mwingine, basi wangeanza kufuatilia mtambo ule tangu wakati ule, si ajabu mtambo ungeshaingia nchini kipindi kirefu na kukabiliana na hili tatizo la sasa la kina kidogo cha maji.

Kikwete na Ngeleja kuna haja ya kufuatilia kuhakikisha $200 milion zilizolipwa na TANESCO kwa papa fisadi Rostam kama malipo kwa kuzalisha umeme zinarudishwa haraka maana Richmond/Dowans hawakuzalisha hata tone moja la umeme.
 
Last edited:

...........Hakuna mtu anayekataa/atakayekataa kitu kilicho genuine na kwa manufaa ya Taifa...........ni hivi watu wanafanya makusudi kutofanya mipango endelevu wakisubiri kufanya mngt by crisis.......hili ndilo tunaloliktaaa.............

Kumbuka issue ya Radar na wahusika wake...........nothing new...watu ni wale wale.............

Tunajua kuwa hali ingekuwa hivi kwani walishasema tena kwa jeuri kuwa kama hamtaki Dowans basi mtakuwa gizani........wakti watu walishatoa solution kibao hapa hapa JF...........au mnasubiri zile solution ambazo zitawanufaisha matumbo ya mafisadi...........inaudhi kwa kweli................halafu unakuta eti watu wanawatetea hawa mapunguani................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…