Pre GE2025 Tanga: Afisa Mwandikishaji Handeni ataka waandikishaji wasaidizi kutunza siri za wananchi watakaojitokeza kujiandikisha

Pre GE2025 Tanga: Afisa Mwandikishaji Handeni ataka waandikishaji wasaidizi kutunza siri za wananchi watakaojitokeza kujiandikisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Handeni Mjini Maryam Ukwaju amewataka waandikishaji wasaidizi,kuhakikisha wanatunza siri za wananchi watakaojitokeza kujiandikisha kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Ukwaju amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi ngazi ya vituo na Waendesha vifaa vya Bayometriki kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata zote 12 za Halmashauri ya Mji Handeni Mkoani Tanga.

Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakaloanza Handeni Mjini kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari 2025 na vituo vitakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.

 
Back
Top Bottom