Wasanii/wanamichezo na vijana wanazidi kuaibisha wakiongozwa na huyu kijana aliyepata nafasi ya kuhakikisha sekta ya sanaa, michezo na utamaduni inasimama vizuri na wasanii wananufaika na kazi zao.
Kila siku ni uchawa left and right! Msanii akiumwa kidogo tu anaanza kutembeza bakuli, kwenye soka uozo kibao. Wachoraji, wachongaji, wapiga picha, etc utafikiri wao wizara haiwahusu, kuna fursa kibao lakini kimya, kutwa kuchwa na shughuli za kichawa. Nay wa Mitego amekuwa kama mkimbizi lakini wala hilo halionekani. Bure kabisa.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo ambaye pia ni mbunge wa Muheza Tanga Hamis Mwinjuma (MwanaFA amesema Kundi la Waendesha magari la SAMIA Four by Four Safari linatarajia kushiriki mbio za magari ya aina hiyo zikiambatana na kufanya Utalii wa vivutio mbalimbali vya mkoa wa Tanga katika wilaya za Lushoto na Muheza kuanzia Februari 21 ikiwa ni sehemu ya kuchagiza ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani humo.
Naibu waziri Mwinjuma (Mwana FA) amezungumza kuhusu mbio hizo jjijini Dodoma na malengo yake na kuwakaribisha wote wenye Magari ya aina hiyo kushiriki.