BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Leo Alhamisi, Septemba 5, 2024 ni siku nyingine ya matumaini kwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Tanga, Kombo Mbwana, anayekabiliwa na kesi ya jinai, kurejea uraiani kwa dhamana.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Mahakama ya Wilaya ya Tanga, kuhusiana na maombi ya Jeshi la Polisi kuomba mshtakiwa huyo asipewe dhamana kwa sababu za kiupelelezi wa kesi inayomkabili.
Kombo ambaye awali aliripotiwa kupotea kabla ya Jeshi la Polisi Tanga, kutangaza kumshikilia siku 29 baadaye, anakabiliwa na kesi ya jinai, akidaiwa kutumia vifaa vya mawasiliano ikiwemo kadi ya simu ya mkononi isiyosajiliwa na bila kutoa taarifa.
Licha ya mashtaka yanayomkabili kuwa na dhamana na Mahakama kutangaza kuwa dhamana yake iko wazi tangu alipopandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka Julai 16, 2024, lakini dhamana yake imekuwa na vikwazo mbalimbali na hivyo kumfanya aendelee kusota mahabusu hadi leo.
Hata hivyo, leo Alhamisi, Septemba 5, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Tanga inatarajiwa kutoa uamuzi wa zuio la dhamana yake lililowekwa na Jeshi la Polisi Tanga.
Pia soma:
- Kombo aendelea kusota ndani, ombi la kupewa dhamana lagonga mwamba, shauri kuendelea August 29, 2024
- Sasisho: Kombo Mbwana wa Tanga akosa dhamana licha ya kutimiza masharti ya dhamani kama ilivyopangwa
- Mbwana Kombo wa Tanga, kada wa CHADEMA bado hajapata dhamana, inadaiwa Mawakili walinyimwa ushirikiano na Hakimu Moses Maroa