Pre GE2025 Tanga wafanya matembezi maalum barabarani ya kumpokea Rais Samia

Pre GE2025 Tanga wafanya matembezi maalum barabarani ya kumpokea Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wananchi wa Jiji la Tanga wamejitokeza kwa wingi kushiriki matembezi ya pamoja yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, Katibu Tawala wa Tanga, Dalmia Mikaya na Mbunge wa Tanga Mjini Ummy Mwalimu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumpokea Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kuwasili Mkoani humo kesho February 23,2025 kwa ziara ya kikazi itakayokamilika March 01,2025.

Snapinst.app_480665460_18489201283057742_965334309190457313_n_1080.jpg
Matembezi hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambapo DC Kubecha amesema Wananchi walioshiriki matembezi hayo wameonesha shauku kubwa ya kumpokea Rais Samia, wakisema kuwa uongozi wake umeleta maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali, ikiwemo miundombinu, elimu, na afya.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga ambapo atazindua na kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na Wananchi.

Snapinst.app_472728263_18489201355057742_5191415279490063904_n_1080.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batlida Burian ni miongoni mwa Viongozi waliowaunga mkono Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga kwa kushiriki matembezi hayo ambapo amesema ni heshima kubwa kwa Mkoa wa Tanga kumpokea Rais Samia na kusema ni wajibu wa Wananchi kujitokeza kwa wingi ili kumpa Rais mapokezi mazuri “Huu ni uthibitisho wa mshikamano wetu na uungwaji mkono kwa juhudi anazofanya katika kuleta maendeleo nchini”

Snapinst.app_475408998_18489201370057742_8630383972891335975_n_1080.jpg
Pia, Soma
 
Back
Top Bottom