Tanga: Yaliyojiri Kwenye mazishi ya Ally Mohamed Kibao, Kiongozi wa Chadema aliyeuawa kikatili

Tanga: Yaliyojiri Kwenye mazishi ya Ally Mohamed Kibao, Kiongozi wa Chadema aliyeuawa kikatili

nightwalker

Member
Joined
Jan 29, 2020
Posts
51
Reaction score
75
Jiji la Tanga limegubikwa na huzuni kubwa mchana huu kufuatia msiba mzito wa ALI MUHAMMAD KIBAO.ALI MUHAMMAD KIBAO alikuwa ni Mtoto wa Sheikh Muhammad Ali Albuhri.

Baba yake mkubwa ALI MOHAMED KIBAO ni Hemed bin Jumaa bin Hemed ambaye amewahi Kuhudumu kama Mufti Mkuu wa Tanzania. Msiba huu ni pigo kubwa kwa familia ya ndugu zetu Waislamu Jijini Tanga na Tanzania yote.Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun. TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

1725880964546.png
1725881042759.png
1725881085652.png
1725881122867.png
Ni zamu ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa wa Tanga kutoa salamu za pole."Hili jambo liwe la mwisho isije kuwa ni mazoea."

1725881212529.png
Mwakilishi wa TLP mkoa wa Tanga"nitoe pole kwa familia na CHADEMA"

1725881427344.png
Ni zamu ya Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga kutoa salamu za pole."Nazungumza kama Mstahiki meya wa Jiji la Tanga,nazungumza kama Diwani wa kata hii,nazungumza kama jirani na Mzee wangu Ali Kibao""Ali Kibao ni maarufu miongoni mwa watu na familia ya watu wa wanaotoka mkoa wa Tanga"."Mambo mengine wenye mamlaka watazungumza,naomba Mwenyezi Mungu awape familia hii subra""Mungu awape Viongozi wa CHADEMA faraja tutumia msiba huu kutuleta pamoja."

1725881471996.png

1725881532680.png
Waziri wa mambo ya ndani Eng.Hamad Masauni ameingia msibani wakati huu.

1725881604542.png
Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Mh.Godbless Lema anatoa salamu za rambirambi."Mheshimiwa waziri huu uwe msiba wako wa mwisho kwenda msibani kwa mtu aliye uuawa kwa kutekwa""Nilitarajia baada ya statement ya Rais Jana wewe utakuwa umejiudhuru na IGP atakuwa amejiudhuru,naongea hivi with due respect bila kukuvunjia heshima""Leo mimi na Boni tumeambiwa tukimaliza mwezi huu bila kutekwa na kuuawa tushukuru Mungu.""ALI MOHAMED KIBAO ajatekwa na Majambazi""Tuache kujali mipira kuliko uhai wa wenzetu"

1725881652962.png
Makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa Mheshimiwa Isiaka Mchinjita anatoa dalamu za pole."Waheshimiwa Viongozi wa CHADEMA niwape pole sana,Msiba huu ukiondoa huzuni kuwa tumepoteza ndugu yetu tumepata hofu kubwa sana.""Waziri wa Mambo ya ndani upo hapa,ndugu yetu ameuawa kwa sababu Jeshi la Polisi limeshindwa kulinda Usalama wa Raia na mali zake..""Mambo haya na matukio haya yanaendelea bila kuendelea kupata majibu""Naungana na Kiongozi mwenzangu Lema,nilitarajia tangu jana ungekuwa umejiudhuru""Sativa baada ya Kutekwa alifikishwa kituo cha Polisi Oysterbay""Tumetoa wito kwa Rais kuunda tume ya Kijaji ili Kukomesha matukio haya.."

1725881728391.png
Katibu Mkuu John Mnyika anatoa salamu za pole."Ali Muhammad Kibao ni Mjumbe wa Sekretarieti na Kwa maana hiyo ni Mjumbe pia wa Kamati kuu ya CHADEMA,Pole sana Mheshimiwa Mwenyekiti Mbowe""Poleni sana familia ya Ali Kibao,nilikuwa naye hapa Tanga tukiwa tumejifungia kupanga mikakati wakati wa Retreat, baadae akaniaga anaenda Dar es saalam"Kwakweli tumepoteza kiongozi mashuhuri, kwa sababu ya uwezo wake wa Kitaalamu wa kazi, naamini mfumo ulikuwa unamfahamu,na wakati vyombo vya dola wanaenda Kumchukua kwenye basi vilikuwa vinajua vinaenda kumchukua nani.

""Namimi naunga mkono wenzangu juu ya uwajibikaji wako wa kujiuzuru nafasi yako ya uwaziri""Nimepata wasaa wa kuwasikia Kondakta,Dereva na watu wengine kwa vyovyote vile ,Idara ya usalama wa Taifa ni wahusika wa tukio hili,uwajibikaji usiishie Jeshi la Polisi tu ""Aki Kibao alikuwa mtu wa haki,na nyinyi Waislamu mnasema kuwa Jigadi iliyo bora ni kusema haki mbele ya watawala dhalimu,tunaomba mtuvumilie kwa namna tunavyo omboleza na Kulia kwetu."

1725881781324.png
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda Buriani amezomewa baada ya kulazimisha kuja Kuongea Msibani kinyume na utamaduni wa dini ya Kiislamu Mwanamke kuja mbele ya wanaume kuhutubu.

1725881832419.png
Waziri wa mambo ya ndani Eng Hamad Masauni akitoa Salamu za pole."Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Tanga,Mstahiki meya,Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mheshimiwa Mbowe,Viongozi wa ACT Wazalendo na Vyama vingine ambavyo sijavitaja..""Naomba nianze na kumshukuru Mwenyezi Mungu.""Mwenyezi Mungu tunaomba Umjalie Mwenzetu Ali Kibao akae mahala pema,na sisi utujalie mwisho mwema,utujalie tuio kaa hapa kuwafariji wafiwa badala ya kuwaongezea majonzi."

Waziri wa mambo ya ndani Eng.Hamad Masauni"Mheshimiwa Rais amehuzunishwa sana na tukio hili""Nitoe wito kwa mtu yeyote kuacha kushutumu,badala yake kama mtu anakielelezo aweze kukiwasilisha""Wanafamilia wajue Serikali ipo pamoja na nyie,na hakuna namna ya kuharakisha utoaji haki""Kwa sasa tumuombee mwenzetu dua,na nina rambirambi kwa niaba ya serikali nitaikabidhi kwa familia baadae"

Waziri Masauni amezomewa na wananchi,wamempokonya maiki amerudi Kukaa Kwanza.

Massuni ametaka kurudi kuongea, Wananchi wanaimba Masauni jiuzuulu,Masauni Jiuzulu,Masauni Jiuzulu,Msauni Jiuzulu..!

1725882128793.png
Mwenyekiti Freeman Mbowe amesimama kutuliza hali ya hewa na Kuwaomba wananchi waruhusu Waziri Masauni amalizie kutoa hotuba yake.

1725882912310.png
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anatoa salamu za rambirambi. Naomba sana Wanafamilia na Masheikh muelewe machungu ya waombolezajiNitawapitisha kwa kifupi safari ya machungu yao.Jamii hii mnayo iona labda imekosa adabu, wamechoka kuomboleza wenzao.Siyo mara moja au mara tatu wamezika viongozi wao au wamepoteza wenzao ambapo hatujui leo walipo.

Wiki kadhaa zilizopita, viongozi wawili na mwanachama mmoja wametekwa mchana kweupe wakiwa wameitwa kufuata pikipiki yao kituo cha polisi Walikuwa Godwin Mlay Katibu wa wilaya Temeke, Deusdedith Soka ambaye ni Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA na Mwanachama wa kawaida Frank Mbise Waliitwa waende Polisi kufuata pikipiki yao na walipokwenda hawajarudi hadi leoMheshimiwa Masauni, wote tumesikia kauli ya Rais, lakini ni kauli ambayo inatuelekeza vyombo vilevile tunavyo vituhumu ndiyo vichunguze, HAIWEZEKANI Wewe kama Mwakilishi wa Rais, mueleze Rais kuhusu Rai ya Waombolezaji kuwa Mheshimiwa Raia anayo mamlaka ya kuunda tume ya Kijaji, aunde tume ya kijaji.Nimechoka kuulizwa na Wazazi...

"Mbowe wapo wapi watoto wapi..?"

Hapa Tanga tu alitekwa kiongozi weru, Kombo Mbwana Twaha mwezi mzima na baada ya kupatikana mnamshikilia Magereza lwa mashtaka yenye dhamana.Leo amani inatoweka msibani, lakini ipo siku amani hii itatoweka mitaa yote ya Tanzania Hii ndiyo Rai yetu, Mheshimiwa aunde tume ya Kijaji, sisi ambao tuna ushahidi hatupo tayari kutoa ushahidi kwa MapolisiAunde tume ya Kijaji tupeleke ushahidi. Nilifanya mkutano wa waandishi wa habari nikawataja na tuna ushahidi mwingine mwingi tu.Tume ya Kijaji ndiyo inaweza kuwabaini na kumshauri Mheshimiwa Rais hatua za kuchukua.Nimesema hasira hii unayo iona hapa, inaweza kuwa barabarani, tukaharibu nchi yetu.

Meddy nimemfahamu nje ya CHADEMA, mwaka 1990 tulifanya wote biashara ya MadiniMtu mwema sana, mtu mpole ambaye huwezi kumpiga hata Kofi ukimtazama.Mmetuondolea roho ya mtu mwema ambaye ni hazina yetu. Tazama magari yote haya kutoka mikoani huko, ni ishara kwamba mmeondoa hazina kubwa sana kwetu.Siku ya Jumatano, kesho kutwa Viongozi wote wa kata zote 112 za Dar es saalam, Viongozi wa Majimbo yote 10 Mkoa wa Dar es Salaam, tukutane Makao makuu ya chama tutakuwa na Jambo letu

Naomba kumaliza kwamba, Damu ya ndugu yetu Meddy ikawe ndiyo mbegu ya kuleta mabadiliko dhidi ya uonevu na ukandamizaji. Asanteni Sana.

Pia, soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Shida ilianzia kwa yule Mama mwenye ushungi mweusi alipokuja na nukuu za Hadithi za mtume kuhusu mtu aliyeuawa na ng'ombe wakati jamii ikidhani ameuawa na mtu.

Hicho kifungu ni kama dharau ku justify mauawaji ya Ally na kwamba watu wasiendelee kunyooshea vidole polisi na vyombo vya usalama kiujumla.

Wamekosea sana
 
Wizara nyeti kama wizara ya mambo ya ndani ya nchi ni vyema na wakati muafaka iongozwe na mtanganyika baada ya maboresho ya katiba.
 
Shida ilianzia kwa yule Mama mwenye ushungi mweusi alipokuja na nukuu za Hadithi za mtume kuhusu mtu aliyeuawa na ng'ombe wakati jamii ikidhani ameuawa na mtu.

Hicho kifungu ni kama dharau ku justify mauawaji ya Ally na kwamba watu wasiendelee kunyooshea vidole polisi na vyombo vya usalama kiujumla.

Wamekosea sana
huyo wanamlawiti.
analeta usenge wakati ni dhahiri jamaa kauwawa na samia na genge lake la ccm
 
Shida ilianzia kwa yule Mama mwenye ushungi mweusi alipokuja na nukuu za Hadithi za mtume kuhusu mtu aliyeuawa na ng'ombe wakati jamii ikidhani ameuawa na mtu.

Hicho kifungu ni kama dharau ku justify mauawaji ya Ally na kwamba watu wasiendelee kunyooshea vidole polisi na vyombo vya usalama kiujumla.

Wamekosea sana
Namuombea radhi Shangazi yangu, kwa kuulinda mkate wake japo batili
 
Shida ilianzia kwa yule Mama mwenye ushungi mweusi alipokuja na nukuu za Hadithi za mtume kuhusu mtu aliyeuawa na ng'ombe wakati jamii ikidhani ameuawa na mtu.

Hicho kifungu ni kama dharau ku justify mauawaji ya Ally na kwamba watu wasiendelee kunyooshea vidole polisi na vyombo vya usalama kiujumla.

Wamekosea sana

..Meya wa Tanga amezungumza kwa adabu.

..Waziri wa Mambo ya ndani, na Mkuu wa mkoa, walikwenda pale kufanya uchawa, na ndio maana kukatokea shida.

..Badala ya kumuomboleza marehemu na kuwafariji wafiwa, wao walikwenda kuitetea serikali na Raisi.
 
Rip Mzee Kibao
Shida ilianzia kwa yule Mama mwenye ushungi mweusi alipokuja na nukuu za Hadithi za mtume kuhusu mtu aliyeuawa na ng'ombe wakati jamii ikidhani ameuawa na mtu.

Hicho kifungu ni kama dharau ku justify mauawaji ya Ally na kwamba watu wasiendelee kunyooshea vidole polisi na vyombo vya usalama kiujumla.

Wamekosea sana
 
Kwanini kaenda!? Ni hatari kwake
Alienda kwa sababu alipewa bahasha ya khaki akaikabidhi wakijua itawapoza, CCM hupenda kutanguliza bahasha kama walivyofanya kwa yule binti mwanafunzi aliyepigwa risasi akiwa ndani ya basi, na yule dereva aliyepigwa risasi na mkuu wa mkoa.
CCM hutembea na mburungutu ya pesa kulainisha njia ili wapite.
 
Back
Top Bottom