Tanganyika groundnuts scheme

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Baada ya vita ya pili ya dunia Uingereza ilipata upungufu mkubwa sana wa mafuta ya kupikia hivyo wakafanya mpango wa kulima karanga ili kutengeneza mafuta. Hapo ndiyo ikazaliwa Tanganyika groundnuts scheme.

Huu mradi ulifeli vibaya sana hadi ikifakiwa mradi wowote wa kijinga unafananishwa na Tanganyika groundnuts scheme. Huu mradi ulifanyika toka mwaka 1947 hadi 1951. Ulipoteza pesa nyingi sana.
Walichagua sehemu ya kulima huko Kongwa dodoma. Walipanga kulima ekari Laki moja na nusu.
Kwanza sehemu waliyochagua ilikuwa na asili ya udongo mfinyanzi, hilo suala lilifanya uvunaji wa karanga kuwa mgumu sana.

Sehemu waliyotaka kulima kulikuwa na mibuyu mikubwa sana. Matrekta waliyoleta yaliharibika vibaya sana wakati wa kusafisha shamba, pia kulikuwa na nyuki kwenye hiyo mibuyu na ziliwauma wengi sana. Hili bila shaka liliwafurahisha sana wazawa maana mibuyu mingine ilikuwa sehemu za kutambika, watakuwa waliamini mizimu imechukia.
Sehemu kubwa ya vibarua weusi walikuwa hawajui kutumia matrekta hivyo waliyaharibu haraka. Wafanyakazi wakaanza kugoma nk. Pia maeneo hayo waliyoweka kambi kulikuwa hakuna maji na Tembo na wanyama wengine waliwasumbua sana.
Mafuriko nayo yalikuja na kuzoa kambi yao. Wanasema hadi mradi unafungwa eneo hilo lilibaki jangwa tupu.
Source wikipedia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…