Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi, wanaovuna ni wachache wakati waliopanda ni wengi

Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi, wanaovuna ni wachache wakati waliopanda ni wengi

Maji Chai

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2018
Posts
265
Reaction score
362
Mwaka 1962 tarehe 9 Disemba Tanganyika ilijitangaza kuwa jamhuri na Mwalimu Nyerere akawa raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Tukawa tumetoka katika wakoloni wa kizungu na kuanza maisha ya ujamaa chini ya nyerere sikuwepo kwahiyo siwezi zungumzia nyakati ambazo sikuwahi kuishi humo.

Februari 5,1977 baada ya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) kuvunjwa kikazaliwa chama kipya na kujiita Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hapa Wakoloni weusi wakawa wamezaliwa.

Aprili 26,1964 Tanzania ikazaliwa baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na Nyerere kuwa Raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi 1985 alistaafu baada kuona nchi imemshinda kutokana na itikadi zake za ujamaa.

Tangu CCM iingie madarakani wamewafanya Watanzania wengi kuwa mazumwamwa na watanzania wamekuwa wapole kwa kipindi kirefu.Lakini kuna muda uvumilivu huwa una ukomo,pengine miaka ya nyuma wamekuwa wakifanya uchafu wao kwa siri kubwa lakini miaka mitatu iliyopita tangu Dr.Samia Suluhu Hassan mfungua nchi achukue kijiti mambo yamebadilika sana.

Kipindi cha kuapishwa chake kelele zilikuwa nyingi sana watu wakajisahau wakahisi wamepata tumaini lililo bora lakini amewastaajibisha na utendaji kazi wake. Nchi imekuwa ya hovyo haijawahi kutokea,utekaji kimekuwa na jambo la kawaida linalofanywa na jeshi la polisi, rushwa imekuwa ni janga la taifa,kodi zinaongezeka kila kukicha watu wakilalamika wanaambiwa wahame nchi.

Kwa mara ya kwanza CCM tangu kuundwa imekosa mvuto kabisa ni kama vile meli inazama kwa kasi.Japo kelele ni nyingi ila Rais yeye anasema amziba maskio kama chura hataki kuskia. Alisema kila mtu ale kwa urefu wa kamba. Ni katika serikali ya Rais Samia polisi wamekosa weledi kabisa na kufanya mambo ya hovyo kabisa.

Wamaasai ndo hao wanatolewa ngorongoro kwa ulazima eti kwasababu kuna waarabu wanataka kujenga hoteli za kifahari. Wanasema bandari ishauzwa,wanasema ndege zinahamishiwa zanzibar,wanasema Abduli kijana wa Rais Samia kawa dalali wa nchi,Wanasema Rais Samia kachukua hongo kutoka kwa Rais wa Zimbabwe, Wanasema Rais alipeleka jeshi kenya kupiga Gen-z waliikuwa wanaandamana,Wanasema ukijaribu kuikosoa serikali majamaa yenye gari nyeusi watakuteka,Wanasema keki ya taifa inaliwa na wachache (Maneno ya walevi wa ile bar)

Ni lini sisi kama Watanganyika maana ndo tunapitishwa kwenye hili tanuru la moto tutaamka kutoka usingizi na kudai haki zetu kutoka kwa hawa wakoloni weusi, ni lini tutasimama na kuzijua haki zetu, ni lini tutasema imetosha ni wakati wa mabadiliko,ni wakati wa tanganyika kuwa huru.

Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi, wanaovuna ni wachache wakati waliopanda ni wengi. Wanasahau sisi ndo tunanunua mbegu,sisi ndo tunamwagilia,sisi ndo tunapalilia ila kwenye kuvuna sisi tumewekwa pembeni.

Watanganyika tuamke.

Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanganyika

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Amka ukutane na virungu
Picha ya mbele siasa nyuma jeshi
Tusipoamka kutoka usingizini wajomba zake Rais Samia watakuwa washaanza kututawala tutarudi enzi za kutawaliwa na akina Sultan. Taifa limeoza hili,tunakoelekea tunaenda wakimbizi kwenye ardhi yetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom