Kwa kuwa mpaka sasa mchakato wa kupata katiba mpya umevurugwa kwa makusudi kukidhii masilahi ya makundi machache katika jamiii haswaa WANASIASA nashauri TLS (Chama cha wanasheria Tanganyika) wafungue kesi kuzuia kuendelea kwa mchakato huo.
TLS wanayo fursa pana ya kufungua kesi hiyo ikiwa ni taasisi ya wasomi wanasheria nchini na wenye kila uwezo wa kuiandaa na kuisimamia kesi hiyo.
Ni wakati muafaka sasa kwa TLS kuonyesha nafasi yao katika masilahi mapana ya kukuza demokrasia nchini.