Tanganyika na Zanzibar tumeungana kisiasa zaidi

Tanganyika na Zanzibar tumeungana kisiasa zaidi

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
974
Reaction score
245
Ifike mahali tuwe wakweli na muungano wetu.

Kuna Faida gani kwa mtanganyika wa Kawaida anayoipata Ktk muungano huu? Nauliza hivi; kuna Faida gani kwa mzanzibar wa Kawaida anayoipata Ktk muungano huu?
Nimeenda Zanzibar kununua bidhaa nilipofika bandari ya Dar nikaambiwa nilipe Ushuru, alienidai kulipa Ushuru aliniambia nimetoka nchi nyingine hiyo, cha ajabu kuna rafiki yangu Yuko Zanzibar anaishi huko Mara nyingi hununua baadhi ya vitu toka bara na kupeleka huko lakini halipi Ushuru akifika bandari ya Zanzibar. Huu sio ubaguzi wa kimuungano?

Wazanzibar wamepewa nafasi za uongozi Tanganyika na wanasimamia mambo ya Tanganyika lakini mtanganyika hawezi hata kupewa ubalozi wa Nyumba kumi Zanzibar.
wanasiasa wanafaida zao wanapata na ziko wazi.

Nadhani kuna haja ya kutengana sasa kupitia katiba hii mpya na kwa Kweli Zanzibar ilishapijitenga Siku nyingi kwa kuvunja katiba ya muungano.
Watanganyika tuamkeni sasa nchi yetu tuisimamishe ionekane kimataifa.
 
Back
Top Bottom