Huo ndo uhalisia.
-kwanini Tanganyika haisikiki vinywani mwa watawala. Tanganyika ndio imepewa jina la serikali ya Muungano.
-Kwa muundo huu wa Muungano, Tnganyika ndio imebatizwa jina na kuitwa serikali ya muungano. Kwa muundo huu , kiuhalisia,
Zanzibar hawapo kwenye Muungano, huwa wanatuma tu watu kuja kushika uongozi huku kwa kivuli cha Muungano ambao haupo. Wana serikali yao, wimbo wao wa taifa, mipaka ya taifa lao, bunge lao, katiba yao, budget yao ya taifa lao,.nk
-Ni aibu ya kila mtanganyika kuona haya kuitaja tanganyika wakati wazanzibari wanaona fahari kutaja Inchi yao ya Zanzibar.
-Mungano huu kiinimacho ni kati ya mambo mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwenye katiba mpya.