Rais wa pili wa Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe anaishi Mji Mwema Dar es salaam, Sheikh Ali Hassan Mwinyi Rais wa awamu ya tatu ya Zanzibar naye anaishi Msasani Dar es salaam, Seif Sharriff Hamad Waziri kiongozi mstaafu na Rais mtarajiwa wa Zanzibar anaishi Dar es salaam! Viongozi wengi wa Zanzibar wanaishi huku kwetu bara. Je Zanzibar hakukaliki? au ndiyo namna ya kuimarisha muungano? Zanzibar wanasema suala la mafuta siyo la muungano, je watanganyika wakisema suala la makazi nalo si la muungano itakuwaje?