Tanganyika Packers toka kiwanda cha kusindika nyama na kuuzwa ndani na nje ya nchi hadi kuwa eneo la kuuziwa udongo wa Mwamposa

Tanganyika Packers toka kiwanda cha kusindika nyama na kuuzwa ndani na nje ya nchi hadi kuwa eneo la kuuziwa udongo wa Mwamposa

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267
Anaandika: Martin Maranja Masese, Mtikila

Tanganyika Packers LTD, Kawe, Dar es Salaam 1945-1975. Kilikuwa kiwanda cha kuchakata na kusindika nyama kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi...

Eneo lote la Mloganzila (Muhimbili) lilikuwa ni eneo la Tanganyika Packers na ndilo eneo lililokuwa linatumika kuwapokea na kunenepeshea ng’ombe...

Walipoletwa kutoka mikoani kwa treni wakiteremshwa stesheni ya Pugu, baada ya mwezi wanaswagwa kupelekwa Kawe kuchinjwa na kuchakatwa...

Kutoka Mloganzila kwenda kilipo kiwanda wakati wa kuswagwa, waingereza waliita COWS WAY (njia ya ng’ombe). Waswahili wakashindwa kulitamka ktk namna hiyo badala yake wakawa wanatamka “KAWE” na ndivyo ilivyo hivyo hadi leo..

Tanganyika Packers (TPL) kilikuwa kiwanda kikubwa, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje mpaka kwa malkia wa Uingereza..

Kilikuwa kiwanda tanzu cha shirika la LEMCO (Liebig’s Extract of Meat Corporation) linalofadhiliwa na Uingereza, ambalo lilianzia miaka ya 1860 Uruguay...

Liebig ni heshima ya baba wa (Organic Chemistry), Justus von Liebig. Jengo la machinjio la LEMCO lipo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.

Sehemu kubwa ya nyama kutoka Tanganyika Packers iliuzwa Ulaya hususani katika nchi ya Uingereza. Watanganyika walipata ajira katika kiwanda hicho.

Kiwanda cha Tanganyika Packers kilijengwa na wakoloni kutoka Uingereza 1945 na kilitoa zaidi ya ajira 2,500 ambapo 1,200 zilikuwa ni ajira za kudumu.

Walifanya kazi kwa shift, walichukuliwa kwa mabasi kazini. 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa.

Kiwanda cha TPL kilizalisha nyama za mabuchani, mafuta ya kutengeneza sabuni, damu ilikaushwa na mifupa ilisagwa na kuwa chakula cha kuku.

Pembe na kwato za ng’ombe zilichemshwa kwenye boiler zikatoa gundi, kiwanda pia kilisindika nyama na maharage kama ox-tail beans, ngozi nk.

Katika vita ya Kagera 1978-1979, kiwanda kilitumika kuwalisha wapiganaji vitani. Chakula cha kusindika kilitoka kiwandani kwenda uwanja wa vita.

Mwaka 1975 Serikali ya Mwl, J.K. Nyerere ilitaifisha kiwanda cha Tanganyika Packers na kukifanya kuwa mali halali ya Serikali ya Tanganyika.

Baada ya Serikaki kutaifisha kiwanda, uzalishaji na ubora wa nyama iliyosindikwa ulipungua kwa kiasi kikubwa sana kwa kukosa utaalam na ufundi.

Serikali walinyimwa leseni ya kusafirisha nyama iliyosindikwa. Walinyimwa (phytosanitary certificate) kuthibitisha ubora wa vyakula vya package.

Waingereza wakawanyima cheti cha ubora na usafi wa nyama inayozalishwa. Soko la Ulaya ambako ndiyo walikuwa wanunuzi wakubwa likapotea.

Soko la ndani likawa gumu kiwanda kikaanza kusambaza nyama zake kwenye mabucha ya ndani ya Dar es Salaam na baadae kiwanda kikafariki 1993.

Taratibu kiwanda cha Tanganyika Packers kikaanza kufariki. Baadaye kilibinafsishwa kwa mbunge wa Kawe, hata hivyo aliishia kuuza mashine na vipuri.

Mbunge wa Jimbo la Kawe wakati huo alitokana na CCM, aliitwa Zainuddin Adamjee. aliposhindwa Kukiendeleza akaamua kung’oa mitambo na vipuri..

Mapaa, madirisha, milango na vifungashio vilipelekwa Mapambano (veterinary) na kupimwa kama vyuma chakavu na mapaa kuuzwa kama bidhaa ya chuma chakavu.

Leo pale Tanganyika Packers palipokuwa KIWANDA kilichotoa ajira zaidi 2000, pamefunguliwa KANISA. Watu wanauziwa udongo na mafuta na maji.

Leo pale Tanganyika Packers watu ndiyo wanakondoo na ng'ombe wa kafara na wanajipekeka wenyewe kuchinjwa. Wananyeshwa maji na kulishwa udongo wakielezwa ni UPAKO wa USTAWI na MAENDELEO ya maisha yao.

Kanisa hilo la MWAMPOSA (wao wanamuita MTUME) linawaombea maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira ili wapate ajira kwa maombi.

Maelfu ya vijana wanakesha na kufunga kwake, wananunua mafuta na maji ya UPAKO wapate KAZI. Yeye huyu MWAMPOSA anajenga hoteli kubwa huko nyumbani kwao MBEYA.

Aliyewaroga watawala na watanzania alikufa zamani na dawa ya kuwasaidia aliitupa katikati ya bahari na haiwezi kupatikana leo au kesho.

Hizi ndizo sera za kiuchumi, mipango na mikakati ya CCM, chama kinachoongoza serikali Tanganyika ktk kuwatoa wananchi ktk ujinga na umasikini wao.

CC: Lucas Mwashambwa MamaSamia2025 Pascal Mayalla JokaKuu Tlaatlaah chiembe ChoiceVariable Etwege DR Mambo Jambo Paul Makonda

MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
 
Kanisa hilo la MWAMPOSA (wao wanamuita MTUME) linawaombea maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira ili wapate ajira kwa maombi..
Wameona Bora kanisa kuliko viwandaaa....

Acha mwamposaa ajipigie Hela zake baada ya miaka kazaa akale bada mbelee km kakobee ....

Tz ya CCM tunasafari ndefuu sanaaaa
 
ccm inaturejesha miaka ya Middle Ages! Badala ya kuja na sera ya kujenga viwanda na kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi!

Wao wameona wawakumbatie manabii na mitume feki, ili waendelee kuwapumbaza wananchi kupitia miujiza yao ya mchongo! Tena kwenye karne hii ya 21!
 
Back
Top Bottom