Tanganyika packers vipi? Nani mwenyewe sasa?

Tanganyika packers vipi? Nani mwenyewe sasa?

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
23,265
Reaction score
17,120
Jana nilipata flat tyre kwenye ile njia mpya mbezi beach next to tanganyika packers.niliiangalia ile mandahari ya eneo lile la kiwanda kile kwa masikitiko makubwa.ni karibu ekari 200 kama sikosei.ni aibu eneo lile kukaa vile.kwa nini serikali isiamue kupageuza a new central business diatrict kupunguza msomngamano city centre?pale ni sawa na eneo lote toka akiba mpaka ikulu.mwaka 2003 kuikuwa na so much hype wakati sumaye anazindua uwekezaji wa adamjee sijui na ikajengwa fence kubwa then jk alipoingia mdarakani mambo yakasimama tena.nchi hii vipi lakini?
 
Siyo hivyo tu..eneo lile hata kama ni la nani, serikali bado inao uwezo ku repossess na kutenga matumizi mapya.Hii inawezekana sana..tatizo ni umimi...kama mtu anaona yeye binafsi hawezi kufaidika hakuna hatua yoyote itachukuliwa.Nakumbuka miaka kadhaa huko nyuma eneo lile liliwahi kugawiwa viwanja kwa wakubwa...kelele zikapigwa sana zoezi likasitishwa.Kwanini wasigawe tena wakawapa watu viwanja hata kama ni kwa kununua kuliko kuliacha vile na nyumba zikiendelea kuchakaa tu? Hao wakazi wa nyumba za PACKERS wanakaa kwa utaratibu gani? wengine wanaendesha miradi yu ufugaji humo! Ama kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
 
Re possession ni suala muhimu. Serikali ilichukue na kujenga nyumba za wafanyakazi wa serikali kuliko kuwajengea boko na bunju kule mbali
 
Kilimo kwanza, ufugaji baadaye. Serikali ikiamka na kukumbuka itakurupuka na kuja na kauli mbiu hiyo ili kuunganisha na kilimo kwanza . We ngoja tuu.
 
Re possession ni suala muhimu. Serikali ilichukue na kujenga nyumba za wafanyakazi wa serikali kuliko kuwajengea boko na bunju kule mbali

Tutake radhi wakazi wa Boko.
 
Sumaye ni kambi nyingine na sera zake na priority zake ni tofauti na hawa mabwana wa epa, richmond, dowans, iptl etc
 
Utamuona mwenyewe muda sio mrefu....maana hawa wahindi wametuzidi maarifa.
 
kama si mbali sema ni kilomita ngapi toka city centre? Kama zinafika 35 siombi radhi?

Kutoka Boko nyumbani kwangu mpaka ofisini, napita city centre nanyoosha kilwa road. Kilometa zinasoma 31. Kwa hiyo city centre to boko ni approximately 26 km. Haya sasa omba radhi.
 
serikali ingepima upya pale na kuweka miundo mbinu ya a pilot city an kuuza hizo plot on condtions kwamba zijengwe economic units like banks,malls na yenyewe ifungue ofisi zake ikiwemo mahakama nk.sasa hivi tunasongamana city centre mahakama,posta,mashule,vyuo vingi viko kule.65% ya watu wanaongia mjini daily si kwa kwenda makazini bali ni shida na maofisi.
 
Back
Top Bottom