Tangazo kwa madaktari wa muhimbili waliogoma

MDAU JR

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
452
Reaction score
82
Daktari Njelekela katoa tangazo hili leo kwa madaktari waliogoma Muhimbili:


TANGAZO KWA MADAKTARI WOTE WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unawatangazia Madaktari wote ambao hawafiki kazini kuwa wanatakiwa kurudi kazini mara moja kwa kujiorodhesha majina yao kwa wakuu wao wa Idara.

Aidha, tangazo hili pia linawahusu Madaktari wote wanaokuja kazini lakini hawafanyi kazi, nao wajiorodheshe kwa wakuu wao wa Idara.

Wakuu wote wa Idara wanatakiwa kuwaorodhesha Madaktari wote watakaofika kazini kuanzia leo (2/Julai/2012) na kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu zilizopo.

Zoezi hili litafungwa kesho tarehe 3 Julai 2012 saa tatu asubuhi.

Tangazo hili haliwahusu Madaktari walio katika Mafunzo kwa Vitendo (Interns).

Dr. Marina Njelekela,Mkurugenzi MtendajiSaa 06:00 Mchana

Nakala: Wakurugenzi - Kwa usimamizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…