Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 82
Kuna tangazo linalorushwa hapa nyumbani Tz Dsm majira ya saa tatu hivi usiku na channel 10 by hakielimu halinipendezi hata kidogo, kama kuna mtu anayeweza kulirekodi nakuliweka hapa itakuwa vizuri zaidi ili wote mlione.
Tangazo hilo linaanza kama hivi.
Asubuhi mabinti wawili albino wako nje ya nyumba mmoja wao amevaa sare za shule na anaelekea shule, binti yule mara yuko barabarani na mbele yake kuna vijana watatu ambao wanaelekea uelekeo atokao wanakaribia kupishana, huyu binti albino anapata hofu kubwa kwa kuwa ni katikati ya barabara tena zile ambazo siyo za mijini na kati ya wale vijana wanaokuja mbele yake mmoja wao amebeba jembe, yule binti anapata woga anakwenda mwisho pembeni ya barabara kwa woga no hofu kubwa, mara ghafla nyuma yake wanaoneka mabinti wengine watatu(siyo albino) wenye amani na furaha tele wasio na woga wala hofu, wanapishana na wale vijana watatu ambao mmoja wao kabeba jembe bila tatizo.mwisho wa tangazo.
My Take:
Tangazo lile linawajengea hofu na woga mkubwa ma-albino badala ya kinyume chake.
Tafadhari kama umeliona tangazo lile na uko pamoja nami naomba kwa pamoja tuwaandikie wahusika wa tangazo hilo HAKI ELIMU waweze kulibadisha au kuliboresha zaidi badala ya kuwajengea hofu albino.
anuani yao pepe ni : info@hakielimu.com
Have got nothing against hakielimu wanafanya kazi nzuri.
MJ