Hili tangazo la ajira nilikutana nalo kwenye group moja la WhatsApp, ila nikawa nimelishutukia kuwa Laweza kuwa la kitapeli baada ya kwenda kwenye website ya TRA kulikosa hilo tangazo, pia kufuatia mfumo Wa email ya mtu kwa kutumia gmail.
Lakini kufuatia ugumu wa maisha na kukaa kitaa muda mrefu ikabidi niapply nikisubiri itakuwaje, matokeo yake ni hayo kwenye hizo picha nilizoaambatanisha!
Hawa jamaa walianza na matangazo ya jiji la Dar, Arusha, Mbeya na Mwanza kuna nafasi za ukusanyaji ushuru mshahara 300,000 wakawa wanatumia mfumo huo huo kila kitu, naona sasa wamehamia idara ya TRA πππ