Kapepo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2015
- 1,066
- 1,194
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawataarifu Wasailiwa wote walioorodheshwa katika tangazo lililotolewa tarehe 29 Mei, 2020 lenye Kumb.NaEA.7/96/01/K/208 linaonyesha Usaili unatarajiwa kuanza tarehe 06 hadi 17 Juni, 2020. Ambao nafasi za kazi walizoomba zimeoneshwa kuwa watafanya Usaili wa Mchujo au Vitendo kuwa wanapaswa kuangalia katika akaunti zao walizotumia kujisajili kwenye mfumo wa maombi ya kazi na kuchukua namba ya usaili waliyotumiwa kwakuwa wataihitaji kuitumia kwenye saili husika.
Sambamba na taarifa hii wahusika wenye usaili wa Mchujo au Vitendo pia wametumiwa ujumbe mfupi kwenye simu zao za kiganjani. Ni vyema kila Msailiwa kuinukuu namba husika kwa usahihi kwa kuwa ndio namba itakayotumika kufanyia usaili husika na kupata matokeo ya usaili.
Tafadhali ukiona tangazo hili, mtaarifu na mwingine unayemfahamu anahusika kufanya usaili huo.
Limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Sekretarieti ya Ajira.
3 Juni, 2020