Tangazo La Maandalizi ya Ndoa

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Posts
4,201
Reaction score
236
Ndugu Jamaa na Marafiki

Sijaingia kijiwe hichi siku nyingi kidogo muda mwingine tuko kwenye vijiwe vingine hongereni kwa mafanikio yaliyofikiwa na kijiwe hichi kwa miezi michache iliyopita mpaka sasa hivi - lakini kuna wale wakongwe siwaoni siku hizi kama Naima , AmazingFriend Na Haika Wale wa DHW naona nao wapo humu siku hizi lakini haijalishi .

Napenda kuwajulisha kwamba natarajia kufunga ndoa mwezi wa 9 Mwaka huu Maandalizi ndio yameshaanza na Tunaendelea Kawaida tu .

Nawakaribisha Kwa Maombi , Michango na Wale wanaopenda kuwa kwenye Kamati Ya Maandalizi Ningependa sana kuwa na watu wa jukwaa hili japo 20 Hivi itapendeza kujenga Undungu na mengine mengi .

Kuhusu hii kamati Nitawasiliana na Invisible Tuone Itakuwaje Au tunaweza kuanza na hapa hapa

Ahsante na Karibuni Tena
 

Heartfelt Congrats!...Ni hatua nzuri sana katika maisha...Oa , utulie, uwaze step ya juu zaidi ya michakato ya maisha!!...Mkuu tuko pamoja, japokuwa wengine tutashindwa kuhudhuria vikao kutokana na umbali, tutawasiliana kwa jinsi zinginezo zozote!..Bblessed in all what you plan!
 
belindajacob ......usafiri huo! haloooo........nimependa vikorombweza itabidi nikutafute unirembe kwa harusi ya shy

hongera sana shy .....mungu akujaalie ndoa njema yenye furaha na vizazi vyema....ameeen
 
Congarts! Mungu akutangulie katka mipango yote, cheers.!
 
Hongera sana Shy,

Kila jambo jema linalofanyika ili kutukuza jina lake basi limebarikiwa na Bwana. Nasi tukiwa tumepata hizo baraka tunakuunga mkono. Karibu sana kwenye chama. Teamo ni shahidi wetu mpya kwamba kwa Yesu kuna raha!!
 
Asante sana Shy tuko pamoja kimaombi zaidi ...Kumbe ulikuwa single miaka yote hiyo...
 
Ahsanteni sana kwa wale ambao waliniandikia Chemba Nitaongea na Invisible ili tupange utaratibu mzuri wa masuala mengine lakini yote heri ahsante sana na tuendele kuwasiliana kupitia majukwaa mengine kama teknologia na sayansi au hoja binafsi
 
Hongera sana Shy, hope hautorudi nyuma katika dhamira yako hii
 
belindajacob ......usafiri huo! haloooo........nimependa vikorombweza itabidi nikutafute unirembe kwa harusi ya shy

hongera sana shy .....mungu akujaalie ndoa njema yenye furaha na vizazi vyema....ameeen

ha ha Gaijin Usijali,nitakuchora henna hiyo siku ya huu mnuso na wewe!..ha ha
Hongera Shy!..
 
ha ha Gaijin Usijali,nitakuchora henna hiyo siku ya huu mnuso na wewe!..ha ha
Hongera Shy!..

..Ama kweli tembea uone..Mi nilidhani ni mabaka ya kuungua moto.kumbe ndo urembo!..huh!...

Mhhh, hata mimi nilishauvaa mkenge na kidogo nimpe pole kwa kuungua moto. Nilidhani bibi alimnasa anaiba mboga akamfunza adabu kwa kijinga cha moto.

Naona hang over inanitesa hadi nasahau kuwa nimewahi kuyaona sana hayo mambo nyumbani kwa Fidel (Chuda)!!
 
ningependa kuwa mwanakamati...bahati mbaya nipo tait Nje ya Nchi..anyway nitumie acc yako nikutumie faranga kidogo
 
Hivi ni lazima kuchangiwa ili uweze kuoa? Huwezi kuoa bila kuwa na kamati ya maadalizi?
 
ningependa kuwa mwanakamati...bahati mbaya nipo tait Nje ya Nchi..anyway nitumie acc yako nikutumie faranga kidogo

Hivi tukituma michango kwa Invisible si atafikisha au lazima ziende direct kwa Shy?
 
Hivi ni lazima kuchangiwa ili uweze kuoa? Huwezi kuoa bila kuwa na kamati ya maadalizi?

Nadhani inawezekana lakini,
1. Watu wengine hawana huo ubavu wa kugharimia harusi bila kusaidiwa
2. Wengine wanapenda tu kuwashirikisha ndugu na jamaa ili kunogesha sherehe (shughuli ni watu, na watu wenyewe ndo ...)
3. Wengine ukiwaita bila kuwaomba michango hawaji, kwa hiyo watu wanaogopa kususiwa shughuli na kutoonekana wanajidai/wanaringa
4. Wengine ni nafasi pekee ya kulipa visasi kwa michango yooote aliyowahi kutoa
5. Kwa wengine hii ndo EPA pekee wanayoiiweza
6. .....n.k.
 
Hivi ni lazima kuchangiwa ili uweze kuoa? Huwezi kuoa bila kuwa na kamati ya maadalizi?

Tulisha sema michango mwisho. Sie tutafunga na kuomba lakini suala la kamati na michango sahau.
 
Hii ni jamii na kuna aina mbalimbali za kuleta jamii karibu zaidi moja wapo ni shuguli za harusi na zingine nyingi sana zinazoleta watu karibu ndio maana nikaomba idadi fulani ya wanachama kama wanaweza kuja kwenye kamati huu ni mwanzo tu huko mbeleni wengine wanaweza kujitokeza na kufanya mengi zaidi but jamii lazima iwe karibu zaidi utamaduni wetu wa kupendana na kuwa karibu lazima udumishwe kwenye shuguli kama hizi
 
Uuum,
Kama sikosei SHY si kuna wakati ulisema unaachana na JF?
Au michango ndiyo imekurudisha humu?
**Just kidding!
 
Mwenyezi Mungu atakuongoza na ndoa yako itakuwa na amani na salama Isha'Allah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…