Wananchi wa Tanganyika ninasikitika kuwatangazia kupotea kwa LUKU ya Mzee Makamba.
LUKU hii ndiyo ilikuwa ikimsaidia Mzee kuchuja pumba na mchele, mbivu na mbichi, moto na baridi, majivu na kaa la moto. Upotevu wake umempelekea Mzee wetu kukosa chujio katika busara na breki mdomoni.
Ilikuepusha maafa makubwa katika matamshi na maamuzi, yeyote atakeiona anaombwa kuikabidhi katika tawi lolote la Chama Cha Mafisadi au Vitengo vya Ubunifu wa Kuwanyonya Wadanganyika (Po-LISI)