Tangazo muhimu kwa watanzania wote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kesho siku ya Jumatano tarehe 23 mwezi Agosti mwaka 2017 kutakuwa na majaribio ya Makombora mikubwa mitatu ambayo itatokea jijini Dar es Salaam ila madhara yake yatatapakaa nchi nzima kutokana na ukubwa wake hivyo Wakazi wote wa hasa Jiji la Dar es Salaam na kwingineko mnatakiuwa kuchukua tahadhari.

Majaribio hayo ya Makombora makubwa matatu yataanzia usawa wa eneo la Kimedani la Msimbazi ambapo yatarushwa katika usawa mdogo wa futi za Bahari kuelekea hasa eneo tengwa la Jangwani ambapo yanategemewa yataanguki hapo na kuleta madhara hayo makubwa matatu tu.

Kwa mujibu wa waliopangwa kuwepo Kesho katika Majaribio hayo ya Makombora wanasema kwamba yataanzia mida ya Saa 11 jioni na kumalizika mnamo Saa 1 usiku ila kutokana na Jiografia ya Makombora kwanza yataanzia eneo la Uwanja wa Taifa kisha yatazunguka angani na hatimaye kupita kwa Kasi sana eneo la Kimedani la Msimbazi na hatimaye kwenda Kutua Jangwani.

Watakaorushwa Makombora hayo matatu watakuwa ni Private Shiza, atafuatiwa na Koplo Laudit na atamalizia Sajenti Emanuel ambao kwa mujibu wa Watu wa Medani wanasema kuwa hawa Warushaji ni Wabobezi hasa ya wa Masuala mazima ya urushaji wa Makombora na huwa wakiyarusha hawakosei na hawajawahi kukosea hata siku moja.

Hivyo basi Watanzania wote mnaombwa kuchukua tahadhari ili yasiwaletee madhara sana.

Akhsanteni.
 
Ukimsikiliza huyu jamaa, unaweza kuwa chizi. Tayari kageuza utafiti wake.
Whatever the case, kesho Omog mechi yake ya mwisho. Mayanja to take charge for the rest of the season.
Sababu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…