Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,168
- 10,810
Naomba msaada wenu wana JF, mimi sio mwana historia lakini kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa, miaka ya 1800 Afrika tulivamiwa na wakoloni kwa sababu kulikuwa na mapinduzi ya viwanda na kuwa walikuja kutafuta malighafi, wakagawa bara letu n.k
Swali langu ni je siku hizi malighafi wanapata wapi?? je Muumba aliumba tena wawe na madini, au wamefungua mashamba ya Mkonge na pamba?? sielewi elewi, maana bado wako juu kiuchumi,sisi wenye malighafi tuko chini kiuchumi.
Ni karne sasa imepita tangu iliposemekana hawana malighafi,
Kama bado hawana wanapataje?? au wamefanikiwaje kuziba hilo pengo liliotokea miaka 100 iliyopita??
nawasilisha
waberoya