The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, amelieleza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa kuelekea miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wilaya hiyo imefanikiwa kupata ofisi yake ya kwanza tangu kuanzishwa mwaka 1978.
Akizungumza katika eneo la ofisi hizo zilizopo Njedengwa jijini Dodoma wakati wa mahojiano na kipindi cha TBC Aridhio, amesema jengo hilo limejengwa ndani ya mwaka mmoja (2023-2024) kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 2.1.
Fedha hizo zimetumika kujenga jengo kuu la ghorofa moja, ofisi ya mlinzi, uzio wa ukuta wa tofali, mifumo ya CCTV, mifumo ya uzimaji moto, viyoyozi, pamoja na kusawazisha ardhi.
Ujenzi huo umetekelezwa na Mkandarasi Azhar Construction Co. LTD na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia BICO.