Tangu awamu hii imeingia madarakani umeme unakatika ovyo

Tangu awamu hii imeingia madarakani umeme unakatika ovyo

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Tangu awamu ya pili iingie madarakani nchi hii imekuwa na changamoto mbalimbali za umeme kiasi kwamba umeme umekuwa kama anasa vile kama bia na sigara.

Yani kila siku nchi yetu inafanya juhudi mbalimbali kuhakikisha kwamba anasa hii ya umeme haiwafikii wananchi kwa wakati.

Kila kukicha ni kuboresha miundo mbinu pale mara kuweka nguzo pale ili mradi tu wananchi wakose anasa hii inayowaondolea msongo wa mawazo kama kilevi.

Inasikitisha sana tangu awamu ya pili iingie madarakani 1985 hadi awamu hii ya sita 2021 kila siku tunaboresha miundo mbinu

Yaani mtaa wangu huu huu ninaoishi tangu 1985 hadi leo 2021 kila siku umeme unakatwa kwa kigezo cha kuboresha muundo mbinu kweli miaka 36 muundo mbinu wa mtaa wangu haujaboreka tuu?

Hizi dili zinazopigwa kwa manunuzi ya kuboreshea muundo mbinu wa umeme mtaani kwangu mnazitumia vibaya kama kila siku mnaboresha tu muundo mbinu.
 
Kama Mwenge siku hizi imekuwa kero tupu,uzalishaji unapungua kila siku.
Makamba alipoapishwa kuwa Waziri wa Nishati aliwapa Tanesco 2 weeks umeme usikatike lakini matokeo yake ni katakata tu.
 
Umeme na miundo mbinu yake, kama kuna shida, nikuboresha miundo mbinu yake, na uzalishaji, si kutimua sijui uongozi, bodi, haviusiani, labda walipenda sura mpya, ila haina maana kwenye umeme!
 
Tatizo
20211117_035906.jpg
20211117_035910.jpg
20211117_035913.jpg
20211117_035916.jpg


Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom