Tangu Deception aanze kampeni yake kuhusu UKIMWI, kuna yeyote humu ndani ambaye amemuamini?

Mzingo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
4,729
Reaction score
10,500
Huyu jamaa kwa muda mrefu amekuwa akieleza kuwa hakuna UKIMWI wala HIV bali ni hoax flani hivi iliyoanzishwa na watu ili kupiga hela. Kwa maana wauze ARV ila hakuna cha UKIMWI wala nini.

Hamaanishi kuwa ukimwi umetengenezwa ili wauze dawa bali hakuna hata huo ugonjwa.

Mimi huwa ninachojiulizaga ''ni kweli huyu jamaa yuko tayari kuchukua damu ya mtu ambaye sisi tunaamini ana HIV na viral load ya kutosha tumchome yeye Deception au tumchukue mdada mwenye ngoma halafu apige bila condom?''

Kwa kweli mimi simuamini, wenzangu nyie vipi?
 
Swali lako linapima hisi za watu, sio uzito wa hoja kitaalamu.
Wamuamini, wasimuamini... Inaleta tofauti gani?
wewe ulivyopima hoja zake uli-conclude vipi?
 
Uzuri wa uhuru wa maoni na mtazamo ni kwamba kila mtu ana anachokiona kipo sahihi na haki hiyo anayo. Muache Deception aamini anachoamini na wewe mkuu kama sisi wengine tuendelee kuwa waangalifu. Mimi binafsi naamini HIV inayopelekea UKIMWI ipo maana nishaona walioteketea sababu ya ugonjwa huu na bado tunawaona.
 
nasubiri kwa maoni yako.
 
nashukuru kwa maoni yako
 
Ukimwi haupo vipi wakati wagonjwa waathirika wapo? Vipimo (vitendanishi) vya kubaini " ngoma" vimejaa maabara?
Watu hadi leo wanaondoka na kg5, af'yeye analeta za kuleta!
Huyo ni wa kupuuza na nadharia zake, kwa kuwa hata hao wagonjwa wa ukimwi tunaowajua hajawabadilishia maelezo maradhi yao,kuwa ni ygonjwa gani unaowasibu,bali kuwadhihaki kuwa ugonjwa unaowatesa siyo ugonjwa na haupo!
Tuelewe nini sasa!
 
Kwa Mtazamo Wangu Huyu Deception Nayeye Ni Mpiga Dili Wa ARVs ndiyo Maana Anashawishi Watu Waamini Hakuna Ukimwi ili Wakiukwaa Awauzie Dawa!!

Kuna Bwege Mmoja Hapa Kitaa alimfata Demu Ambaye Ni Mwathirika Na Sote Mtaani Tunajua Hilo! Sasa Huyu Mchizi Alimfata Doctor mmoja Uchwara Akamwambia Yule Mdada Hana Ngoma Bali Ana Typhoid,, Mchizi si Kaamini Kuwa Hana Ngoma Akenda Akagonga Mzigo!!!
Tulimzika Mchizi Fasta na Kilo Zake 5kg, Demu mpaka leo Adadunda Kitaa.

Sasa Huyu Deception Sijui Ataniambia Nini Wakati Nimewashuhudia Face-to-face Victims Wanakufa Kwa Ngoma.
 
kwa nini unahisi yule jamaa alikufa fasta na kl 5 na yule Dem yupo mpaka leo?
 
Mimi nimemuelewa sana.. Nachukua tahadhari ila suala la kwenda kwenda kupima halipo kichwani mwangu, siji kufanya tena huo ujinga!!
 
Kweni kupiga bila kondom ndo kupata HIV?
 
Kweni kupiga bila kondom ndo kupata HIV?
kunakuwa na probability ya kuupata,tufanye 0.7(70%)

kwa vile yeye anasema hukuna HIV basi yeye uwezekano ni 0(0%)
Hivyo aende kama anaamini ayasemayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…